Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia Hussein Ramadhani (30), Mkazi wa Sinza baada ya kumkamata Vingunguti akiwa amevaa sare za za Jeshi la Polisi (Jungle Green) akijifanya Askari Polisi na kukamata Watu huku wakati mwingine akijihusisha na matendo ya unyang`anyi wa kutumia nguvu akiwa amevaa sare hizo.
"Upekuzi zadi ulimkuta akiwa na vifaa vingine kama Buti za Jeshi la Polisi, kadi za Benki NMB na CRDB, kadi ya Mpiga kura na kadi za NSSF zenye jina la Florence Victor Kiondo ambazo zinachunguzwa jinsi alivyozipata na kuhusishwa na tukio la kihalifu"
"Kumbukumbu zinaonesha Mtuhumiwa huyo alishawahi kufungwa kwa makosa mbalimbali na taratibu za kisheria zina fanyika ili kumfikisha tena Mahakamani, Mtuhumiwa alishawahi kufungwa jela miaka 4 kwa kosa la Kujeruhi akatumikia kifungo katika Magereza ya Mkuza Kibaha, Rwanda Mbeya na kumalizia kifungo Gereza la Kitai Mbinga Mkoani Ruvuma
"Mtuhumiwa alishawahi pia kuhukumiwa kifungo cha nje miezi 6 na Mahakama ya Mwanzo Buguruni kwa kosa la wizi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam litaendelea kufuatilia Watu mbalimbali wanaojifanya Watumishi wa Mamoaka za Serikali na kuwabughudhi Raia wakati wao sio Mamlaka hizo husika" Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Muliro Jumanne