"Kwa upande wa tozo Bilioni 7 tumezielekeza kwenye Sekta ya Elimu Msingi, na hapa tumejenga madarasa 560 na kwenye hili napenda kufafanua kwasababu kuna sintofahamu kwamba fedha za tozo zinaenda kufanya nini na fedha za mkopo zinaenda kufanya nini!?, fedha za tozo tulizopokea Bilioni 7 tumekwenda kukamilisha ujenzi wa maboma ya madarasa 560 ili kuwaunga mkono katika maeneo mbalimbali ambao wametumia nguvu kazi yao kujenga maboma ya madarasa, maboma haya yapo zaidi ya Elfu 10 kwahiyo hata hii fedha ambayo tumepeleka ni ndogo"
"Takwimu zinaonesha mwakani ndio tutakuwa na Wanafunzi wa kwanza ambao wataanza Sekondari kufuatia sera ya Elimu bila malipo, mwakani wakifaulu kwa kiwango cha 82% tutakuwa na ongezeko la Wanafunzi wa Kidato cha kwanza zaidi ya Laki 7, Rais usije ukakatishwa tamaa katika kutafuta fedha kwa ajili ya kutatua kero za Watanzania kwasababu mahitaji ni makubwa sana"
"Mh. Rais sambamba na fedha nyingi ambazo unatupatia kutoka kwenye vyanzo mbalimbali tutasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri, katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Mamlaka za Serikali za Mitaa zilipanga kukusanya Tsh.Bilioni 863.85 na hadi November 30,2021 zimekusanywa Bilioni 356.72 kati ya lengo la kukusanya lengo ambalo tulijiwekea"
"Ujumbe wetu kwako Rais pamoja na Watanzania ni kwamba hatutokuangusha, nakushukuru Rais kwa jinsi unavyoguswa kwa kutatua haraka changamoto za Watanzania, nawashukuru pia Viongozi wengine na Watanzania wote" ——— Waziri Ummy mbele ya Rais Samia Ikulu Dar es salaam leo