Makapuku Forum

Makapuku Forum

MENEJA AFUNGUKA ISHU YA SAIDO
.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema timu yao imeshafika Songea baada ya kuondoka Dar na jumla ya wachezaji 24, huku akithibitisha kuwaacha nyota wanne akiwamo Saido.
.
“Nyota wote walioondoka na timu wapo kwenye hali nzuri ya mchezo na wanawaheshimu wapinzani wao wamejiandaa kwa ajili ya kuendeleza mazuri waliyoyafanya katika michezo miwili ya mwanzo,” amesema.
.
“Kuhusu walioachwa wote ni majeruhi isipokuwa Saido aliyeshindwa kufanya mazoezi na wenzake tangu amerudi kutoka kuitumikia timu yake ya taifa, hivyo kocha Nabi hajaona umuhimu wa kuondoka naye kwenda kwenye mechi hiyo ya kesho kwenye Uwanja wa Majimaji.”

………………….
Screenshot_20211018-162134_Instagram.jpg
 
VARANE WA SIMBA ATAJWA KIKOSI BORA CONGO
.
Beki mpya wa Simba, Henick Inonga Baka ‘Varane’ amechaguliwa Beki Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya DR Congo.
.
Katika kipengele cha beki bora, Inonga amewashinda Ernest Luzolo aliyekuwa AS Vita msimu uliopita, na Nathan Idumba aliyekuwa akiichezea FC Lupopo.
.
Jean Baleke ameibuka kidedea kwa kuchukua tuzo mbili ikiwa ya mchezaji Bora wa ndani na mfungaji bora akimaliza na mabao 14. Wengine walioshinda tuzo ni aliyekuwa Kocha Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge (Kocha Bora), Simon Ommossola wa AS Vita ameibuka kipa bora huku Koffi Kouame wa TP Mazembe akiibuka kiungo bora na nyota wa Maniema Union Maxi Mpia akiibuka mchezaji bora wa jumla na kubeba tuzo ya Ballon d’Or ya nchi hiyo kwa msimu uliopita.
.
Hata hivyo, waandaaji wa tuzo hizo Vodacom League 1 wametoa kikosi bora cha msimu jana ambao ni Omossolo, Djo Issama, Luzolo, Idumba, Inonga, Kouame, Lilepo, Maxi, Baleke Karim Kimvuindi na Mercey Ngimbi ambaye katika dirisha la usajili alihusishwa na Simba na Yanga.

……………
Screenshot_20211018-162440_Instagram.jpg
 
SAIDO HALI ISHAKUWA MBAYA
.
Kocha Nasreddine Nabi amezidi kumtupa nje kiungo mshambuliaji kutoka Burundi, Saido Ntibazonkiza.
.
Saido amekuwa hana namba kikosi cha Nabi, na kwenye msafara wa Songea uliondoka jana asubuhi, nyota huyo wa kimataifa ni miongoni mwa wachezaji wanne walioachwa jijini Dar es Salaam.
.
Kuachwa kwa Saido kunazidi kumpa wakati mgumu Jangwani, kwani hali ni tofauti na ilivyokuwa aliposajiliwa akitokea Vital’O ya Burundi na alikuwa akianza na kuifungia timu hiyo mabao manne na kuasisiti matatu.
.
Yanga imetua Songea ikiwa na Wachezaji 24, huku Saido, Yassin Mustafa, Dickson Ambundo na Mapinduzi Balama wakiachwa kwenye msafara huo.
Screenshot_20211018-162721_Instagram.jpg
 
POGBA AHOJI MBINU ZA SOSHA
.
Hali ishakuwa mbaya. Ole Gunnar Solskjaer presha inapanda, presha inashuka. Kibarua chake kimekaa vibaya huko Old Trafford.
.
Sasa supastaa wake mwenyewe ameanza kuhoji uwezo wa mbinu zake wakati timu ikiendelea kufanya ovyo ndani ya uwanja. Kiungo ghali kabisa kwenye chama hilo, Paul Pogba amezidi kumpandisha presha Kocha Solskjaer baada ya kusema:
.
“Tulistahili kufungwa na tunahitaji kubadilika. Tumekuwa na mchezo wa aina hii kwa muda mrefu sana na hatujamaliza tatizo, tunafungwa kirahisi sana, mabao ya kijinga.
.
“Mashabiki wanatupa hamasa, wanatupa presha na mambo mengine kama hayo. Tunahitaji kukua, kucheza kwa uzoefu zaidi na katika namna nzuri.
.
“Tunahitaji kufanya kitu, tunahitaji kubadilika. Kwa sasa tunahitaji kutafuta suluhu ya mechi tunazopoteza, kwa sababu tulistahili kupoteza. Inavuruga sana. Tunahitaji kutafuta akili sahihi na mbinu sahihi.”
.
Kocha Solskjaer alikiri kufanya makosa makubwa ya kumrudisha kwenye kikosi beki Harry Maguire, wakati nahodha huyo alikuwa na siku moja tu ya mazoezi akitokea kuugua maumivu ya misuli.

……………….
Screenshot_20211018-162904_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Juzi kwenye mchezo kati ya Inter Milan na Lazio kulikuwa na tukio Kati ya Joaquin Correa wa Inter Milan na Luiz Felipe wa Lazio

Baada ya dakika 90 za mchezo ambapo Lazio alishinda 3-1, Luiz Felipe alitoka mbio na kwenda kumrukia Rafiki yake Correa ambaye sasa yupo Inter Milan

Kumbuka kuwa Correa msimu uliopita alikuwa Lazio ila msimu huu amehamia Inter Milan, kumbuka pia wawili hao ni Marafiki wakubwa sana

Luiz Felipe alichotaka ni kumtania Rafiki yake baada ya hayo matokeo ya mwisho! Ila Correa aligeuka kwa hasira na kupelekea ugomvi Mkubwa sana uwanjani na Felipe akapewa kadi Nyekundu

Felipe alilia sana baada ya kupewa kadi nyekundu hiyo tena kutokana na tukio alilomfanyia Rafiki yake Kipenzi ila akamgeuka na kujifanya hamfahamu na akapewa kadi

Felipe alilia sana kwakuwa Correa ni Rafiki yake mzuri na walicheza wote msimu uliopita Lazio, familia zao yani watoto na Wake zao ni Marafiki wakubwa sana

Felipe analia kwakuwa timu zimetenganisha picha yao kubwa na nzuri waliyonayo nje ya mpira, analia sana kwakuwa anahisi Rafiki yake amemsaliti mbele ya Refa na amepewa kadi nyekundu

“Ni Rafiki yangu mzuri ambaye mpira wa miguu umenipatia, ila sina cha kusema zaidi ya kuomba radhi “ kauli ya Luiz Felipe

Kuna la kujifunza hapa! Hakuna Rafiki wa kudumu wala hakuna adui wa kudumu Bali kuna maslahi ya kudumu pekee! Rafiki anaweza kuwa nyoka pia[emoji120]
Screenshot_20211018-164939_Instagram.jpg
Screenshot_20211018-164958_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Wakati mchezo wa Newcastle dhidi ya Tottenham Hotspurs unaendelea dakika ya 40 ulisimama ghafla

Shabiki aliekuwa jukwaani akitazama mechi hiyo alipata hitilafu ya kiafya huku ikisemekana kwa taarifa za awali kuwa ni shida ya moyo

WachezAji wawili wa Tottenham Eric Dier na Sergio Reguillion ndio walikuwa wa kwanza kushtuka hivyo walifanya uungwana Mkubwa sana

Eric Dier alitoka mbio sana mpaka kwenye bench la Tottenham na kuwainua Madaktari waende kwa haraka kutoa Huduma huku akisisitiza waende na defilibrator

Wakati huo Sergio Reguillion alimfuata Refa wa mchezo huo kuwa asimamishe kwa muda ili Shabiki yule apate Huduma sahihi uwanjani

Madaktari wa timu zote mbili na wale wa dharura uwanjani wakafika eneo la tukio kuhakikisha wanaokoa maisha ya Shabiki yule kwa haraka sana

Refa alimfuata Steward akiwa na Reguillion kuulizia hali ya Mgonjwa kisha akashauriana na wenzie wasimamishe mchezo na kuendelea kwa mchezo itategemea na afya ya Shabiki yule

Mashabiki wa timu zote mbili wakawa wanapiga makofi kuwapa moyo Madaktari wakati wanaokoa maisha ya mwenzao

FOOTBALL IS FULL OF FAIR PLAY[emoji3531]
 
Back
Top Bottom