Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211014-065336_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20211014-065347_Opera%20Mini.jpg
 
Polisi nchini Kenya wanawashikilia Polisi waliokuwa zamu kwenye kituo cha Jogoo Road eneo la Eastlands Jijini Nairobi baada ya kufanya uzembe uliopelekea Masten Wanjala, aliyekiri kuwaua zaidi ya Watoto 10 nchini Kenya, kutoroka kwenye kituo hicho alichokuwa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani kufuatia matukio yake ya mauaji.

Polisi wamesema wameanza pia msako mkali kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya polisi kubaini hayupo rumande wakati walipokuwa wanaitisha majina asubuhi, Wanjala alikuwa anashikiliwa baada ya kukiri kufanya mauaji mfululizo ya Watoto yaliyolishtua taifa la Kenya na bado haijajulikana aliwezaje kutoroka.
Screenshot_20211014-192309_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amefungua kiwanda kipya cha kutengeneza mabati kiitwacho Taishan Mabati kinachopatikana eneo la Unga Limited Arusha ambacho hadi sasa pamoja na upya wake tayari kimetoa ajira kwa Watu 100 ambapo Raia wanne pekee ni Wachina na wengine waliobaki ni Watanzania.

Baada ya kuona Watanzania wengi wamekubali mabati ya kiwanda hicho kutokana na ubora, kudumu muda mrefu pamoja na bei rahisi huku wakinunua mabati hayo katika matawi yake ya Dar es salaam na Mbeya, Uongozi wa kiwanda hicho umeamua kufungua kiwanda Arusha ili kuwahudumia pia na Watu wa Kaskazini mwa Tanzania.
Screenshot_20211014-192447_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani akiwa Chato leo amesema Serikali inakamilisha vigezo vinavyoruhusu Chato kuwa Mkoa ——— "haujawa bado Mkoa kuna vigezo kadhaa ambavyo bado tunaendelea kuviangalia na vigezo hivi vikikidhi tutalimaliza jambo hilo"

"Tumekuja Chato kwa lengo la kumuenzi Hayati Magufuli, ni mzaliwa wa hapa Chato na kwa hakika alipapenda sana na sisi tunaendeleza upendo wake"

"Nafahamu yapo mambo ambayo Hayati Magufuli aliwaahidi Wana Chato wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 ikiwemo upanuzi wa Bandari, kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege Chato, Hospitali ya Wilaya, VETA pamoja na Stendi, nawahakikishia miradi yote itatekelezwa"———Rais Samia
Screenshot_20211014-192538_Instagram.jpg
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipozuru Kaburi hilo leo Oktoba 14,2021.
Screenshot_20211014-192741_Instagram.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt.

John Pombe Magufuli wakati alipozuru Kaburi hilo leo Oktoba 14, 2021, alipokuwa njiani akielekea katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kushiriki katika kilele cha mbio maalum cha Mwenge wa Uhuru.
Screenshot_20211014-192943_Instagram.jpg
 
Mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kutokana na kukabiliwa na majeruhi ya nyama za paja.

Simba inatarajia kuondoka kesho mchana kwenda Botswana tayari kwa mchezo huo.
Kocha Didier Gomes amesema Mugalu hatakuwa sehemu ya mchezo huo kwani hajafanya mazoezi na wenzake.
Gomes amesema Yusuf Mhilu atakosekana kwasababu ya kuchelewa usajili wa kimataifa.
Screenshot_20211014-193228_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, Kalisti Lazaro amesema Wilaya hiyo imetengewa kiasi cha fedha sh.3.4 bilioni za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.

Hayo aliyasema wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya kisiwani na Kata ya Mayo katika Halmashauri ya Bumbuli ambapo alisema Fedha hizo ni sehemu ya 1.3 trilion zilizotolewa na serikali hivi karibuni.
Screenshot_20211014-193342_Instagram.jpg
 
Mara baada ya kuwepo taarifa za baadhi ya watu kuuza albamu ya msanii wa Bongofleva, Alikiba 'Only One King' mtaani, Serikali kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) imekemea vikali hilo na kusisitiza kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Cosota, Doreen Anthony Sinare, watakaokamatwa kwa kufanya hivyo adhabu iliyoainishwa na sheria ni Sh20 milioni au jela miaka mitano.

"Hivi karibuni baada ya mmiliki wa rekodi lebo ya Kings Music na msanii wa muziki, Alikiba kutoa taarifa ya kupatikana kwa albamu yake ya 'Only One King' katika majukwaa mbalimbali ya mtandaoni ya kusambaza muziki 'Digital Platform' kumeibuka watu wanaodurufu na kuuza mitaani pasipo makubaliano yoyote na yeye hii ni kosa kisheria" amesema Sinare na kuongeza.

"Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki namba 7 ya mwaka 1999 imeeleza kuwa kusambaza kazi ya mbunifu yeyote bila ridhaa yake ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini isiyopungua Sh20 milioni au kifungo cha miaka mitatu mpaka mitano au vyote kwa pamoja," imeeleza taarifa hiyo.

Utakumbuka albamu ya 'Only One King' ilitoka Oktoba 7, 2021 ikiwa na nyimbo 16 ambazo amewashirikisha wasanii zaidi ya 10 kutoka Tanzania, Kenya, Nigeria, Afrika Kusini na Ghana. Hii ni albamu ya tatu kwa mwimbaji huyo baada ya Cinderella (2007) na Ali K4Real (2009).
Screenshot_20211014-193654_Instagram.jpg
 
Takwimu za Azam FC katika mashindano ya CAF CONFEDERATION CUP (Kombe la shirikisho Afrika) tangu walipoanza kushiriki mashindano hayo mwaka 2013.
Screenshot_20211014-193855_Instagram.jpg
 
"MO Salah anafahamu vyema kuwa hakuna mashabiki wanaompenda kama Mashabiki wa Liverpool" Ian Rush, Legend wa Liverpool

Akimpa maneno Salah kuhusu kuongeza mkataba mpya ndani ya Liverpool
Screenshot_20211014-194022_Instagram.jpg
 
Pichani ni Kiungo wa mali, Samir Nasri ambaye alitangaza kustaafu soka mwezi uliopita akiwa na miaka 34 tu

Jana alicheza mechi ya hisani kwa ajili ya watu wa Ivory Coast akiwa na uzi wa Marseille

Nini kimemtokea Fundi Nasri?? Mbona mapema
Screenshot_20211014-194150_Instagram.jpg
 
PYRAMIDS FC [emoji1093] tayari wametua salama Dar es Salaam [emoji929] [emoji1241]
.
AZAM [emoji739] PYRAMIDS
[emoji1001] Jumamosi
[emoji354] 09:00 mchana
[emoji909] Azam Complex
Screenshot_20211014-194917_Instagram.jpg
Screenshot_20211014-194939_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom