Makapuku Forum

Mechi [emoji2391]
Ushindi [emoji2391]
Alama [emoji2397]

Mikel Arteta wa Arsenal ndie Kocha bora EPL mwezi Septemba

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwangu kucheza timu ya Taifa ilikuwa ni kila kitu, bahati nzuri nilianza kucheza tangu timu za Taifa za vijana kwa hiyo nilianza kuwa na hamu ya kuwa mchezaji wa timu ya Taifa. Na huko unakoanzia hakuna kitu zaidi ya ile fahari tu ya kucheza timu ya Taifa.

Kwa mchezaji kupigiwa wimbo wa Taifa ni kitu ambacho huwezi kukutananacho kama haupo timu ya Taifa. Wakati mwingine kuna vitu navipa thamani kuliko hata pesa, ndio vilikuwa vinanipa chagizo ya kufurahi au kusikitika ninapokuwa nje ya timu ya Taifa.

Zamani vilabu vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa vilikuwa vinapigiwa nyimbo za Taifa lakini waliondoa kwa sababu kuna nyakati unakuta karibu wachezaji wote wageni halafu wanapigiwa wimbo wa Taifa.

- Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani Taifa Stars
 
'Chaboli' Jack Wilshere akiwa mazoezini London Colney ambavyo ni viwanja vya mazoezi vya Arsenal

Arsenal wamemruhusu Kijana wao atumie miundombinu yao kipindi hiki anajiweka sawa na akiendelea kusomea Ukocha

Mtoto karejea nyumbani na jezi wamempa za mazoezi FOOTBALL[emoji119]

Wakati huku kwetu Magwiji hata tiketi ya uwanjani hawapewi
 
The Magpies hao Newcastle United ina wamiliki matajiri zaidi duniani wakiwapiku PSG ambao walikuwa wanaongoza

Newcastle - £320 Billion
PSG -£220 Billion

Arab [emoji383]
 
"Kiungo wa Taifa Stars, Mzamiru Yassin atakosa mechi ya Jumapili dhidi ya Benin kutokana na kuwa na kadi mbili za jano. Pengo lake litazibwa na Zawadi Mauya.
.
“Mzamiru ana sifa moja kubwa nayo ni kujituma. Huyu ni punda wa timu...haoni tabu kupigwa chenga, kuingiza mguu sehemu ngumu...ni mzuri zaidi kwenye interception. Ni pengo kwa Taifa Stars.

- Michael Mwebe.
 
Hatma ya Pogba Man United Kizungumkuti !!
.
Kiungo wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba amefunguka juu ya hatma yake na uwezekano wa kurudi Juventus
.
“Ninapapenda Torino! huwa nazungumza na marafiki zangu wa zamani wanaocheza Juve kama Dybala. Kwa sasa nipo Manchester, niko chini ya mkataba hadi Juni 2022 baada ya hapo tutaona nini kitatokea. Nataka kumaliza msimu huu kwa kiwango bora - ndipo tunaona ”.
.
Ikumbukwe kuwa United tangu Julai inambembeleza Pogba kuongeza mkataba wenye mshahara mnono lakini mwamba Paul Labile bado hajakubali kusaini.
 
Hii ni habari nzuri sana kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaotegemea kufika UK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…