"Ndege zina uwezo wa kubeba Abiria 132 na Abiria 12 ni wa daraja la biashara, Ndege zina uwezo wa kuruka saa 6 bila kutua ikiwa na Abiria pamoja na mizigo"
"Shirika la ndege Tanzania (ATCL) linafanya safari katika vituo 13, pia shirika lipo katika hatua za mwisho za kuanzisha safari za muunganiko (connectivity) za Dodoma-Mwanza na Zanzibar-Pemba"
"Air Tanzania imefanikiwa kufungua vituo nane nje ya nchi, Bujumbura (Burundi), Entebbe (Uganda), Guangzhou (China), Ahaya (Comoro), Harare (Zimbabwe), Lusaka (Zambia), Johannesburg (Afrika Kusini) na Mumbai (India) "
"Air Tanzania inatarajia kuanzisha safari za kimataifa kwa vituo vipya ikiwemo Lubumbashi (Congo), Nairobi (Kenya) na Ndola (Zambia)” asema Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi mbele ya Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi leo Zanzibar wakati wa mapokezi ya Ndege hizo mbili.