Makapuku Forum

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu Faiza Salim amesema Wilaya yake imemaliza idadi yote ya chanjo 3320 ya uviko 19 walizopatiwa awali na Serikali kwaajili ya Wananchi na wameonekana wakisherehekea kama inavyoonekana kwenye video.

Faiza amesema kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo iliona kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa Wananchu ili kutambua kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara kama ambavyo kumekuwa na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.
 
Imetokea ajali ya lori Mbagala Dar es salaam ambalo limeacha njia likagonga daladala na kisha nyumba iliyokua pembezoni, baadhi ya Wananchi wamechukua cement iliyokua kwenye lori hilo na kuondoka nayo, taarifa kamili kukujia.
 
UNAAMBIWA

Picha hii ya Cris Froese (41) wa Poland ambayo inamuonesha Mtu akiwa kama amebeba mwezi kisha akauingiza ndani ya gari na kuondoka inatajwa kuwa moja ya picha bora zilizowahi kupigwa.

Cris anasema ilimchukua miaka miwili kuiandaa idea ya kupiga picha hizo na wakati anapiga alikaa mbali kidogo akawa anawasiliana kwa simu na Mwanaume anayeonekana kwenye picha ili aweke pozi sawa hadi walipofanikiwa kupata picha.
 
UNAAMBIWA

Kitabu cha Guinness ambacho hutunza kumbukumbu za rekodi za dunia za vitu visivyo vya kawaida kimemuonesha Mbwa anayeitwa Lou anashikilia rekodi ya Dunia ya Guinness ya kuwa Mbwa anayeishi mwenye masikio marefu.

Mmiliki wa mbwa huyo Paige Olsen wa Oregon Marelani amesema masikio ya mbwa huyo yana inch 13.38 na yanaweza kukutana na hata kufungwa pamoja.
 
UNAAMBIWA

Kutana na Robot mfano wa Mbwa aliyepewa jina la Astro, Robot huyu ana uwezo wa kuzoom kila pande ya nyumba yako kwa kutumia camera iliyofungwa na kukupatia taarifa ukiwa mtaani au Ofisini kuhusu kinachoendelea nyumbani .

Robot huyu ambae atauzwa kuanzia mwishoni mwa mwaka huu kwa $ 999 (Tsh. milioni 2.3) ana uwezo pia wa kusave kile ambacho ungetamani kisipotee.
 
UNAAMBIWA

Chuo Kikuu cha Ryerson nchini Canada kimekamilisha mchakato wa kuanza kufundisha somo la maisha na muziki linalowahusu Wasanii maarufu waliozaliwa Toronto, Canada ambao ni Drake na The WeekEnd.

Taarifa iliyotangazwa rasmi na Chuo hicho kinachotoa pia mafunzo ya Sanaa na Ubunifu, ilisema course hiyo itaitwa 'Deconstructing Drake & The Weeknd' na itaanza kutolewa kwenye muhula mpya utakaonza January mwaka 2022.

Course hiyo itafundishwa na Prof. Dalton Higgins "Ni wakati wa kuwafanya Wasanii wetu wa Rap na R&B kutambuliwa na kupewa heshima wanayostahili na kuruhusu Watu kuwasoma na kuusoma muziki wa nyumbani uliowakuza na kuwafanya wawe maarufu leo"

 
Waziri wa Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80 na zilizobakia mikoani hivi sasa ni chache.

Jumla ya chanjo milioni 1.058 zilizopokelewa nchini kutoka nchini Marekani Julai 24, 2021 na uchanjaji ulizinduliwa rasmi Julai 29, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo imekuja baada ya Serikali kuanzisha kampeni maalum ya kuhamasisha uchanjaji wa chanjo hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo makanisani na kwenye mikusanyiko ya watu.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 4 2021, wakati akifungua kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Neec).

“Tunalo zoezi la uchanjaji. Namshukuru Mungu tumefikia asilimia 80 na kitu huko, tumebaki na chanjo chache sana kwenye mikoa hiyo. Kila mmoja awahi huko na kama kuna mahitaji tutaleta nyingine malengo ni afya,”amesema.
 
Rais wa TFF, Wallace Karia amesema walimuombea Kibu Denis uraia kwa kuwa walikuwa wakimhitaji kwenye medani ya soka nchini.

“Sisi tumemuombea Kibu uraia kwa kuwa tunamhitaji, kwa maelezo mengine ni jukumu la Uhamiaji,” alisema Karia kwa ufupi bila kutaka kufafanua kabla ya hapo alikuwa raia wa nchi gani na ilikuwaje alicheza soka kwa miaka yote na hata kuitwa Stars ilihali hakuwa raia wa nchi.
 
Wakati binadamu wa kawaida akikadiriwa kuwa na urefu wa futi 5 hadi 5.5, hali ni tofauti kwa Julius Charles, mwenye urefu wa futi 7 na inchi 5.

Julius (26) kwa sasa huenda akawa ndiye binadamu mrefu zaidi Tanzania, ukiachana na rekodi ambayo alikuwa akiishikilia mchezaji wa kikapu maarufu wa Kitanzania, Hasheem Thabiti ambaye ana urefu wa futi saba na inchi tatu.

Julius mbali na kimo hicho kirefu, viganja vya mikono na shingo yake vyote vina urefu usio wa kawaida. Anataka kufanana na twiga kwa mvuto wa shingo yake.

Lakini Julius bado ana sifa nyingine za ziada. Ukimkaribia unakutana na binadamu mwenye misuli mikononi iliyotuna mishipa yake.

Unajua analazimika kuvaa viatu vya ukubwa gani? Julius kwanza anavaa viatu saizi 18, sawa na namba 56 na hulazimika kuviagiza nje ya nchi!
Mama mzazi wa Julius, Rachel Joram anasema:

“Nilimzaa Oktoba 28, 1995 mjini Chato akiwa na uzito wa kilo tisa. Ilikuwa ni ajabu lakini walisema hata marehemu babu yake ‘Mgini’ ambaye alikuwa mrefu sana pia alizaliwa na uzito mkubwa.”
 
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ameapishwa kuendelea kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kuteuliwa na Baraza la Wawakilishi la Watu.

Wengine walioteuliwa na baraza hilo ni pamoja na Tagese Chafo ambaye ataendelea kuwa kuwa Spika wa baraza na Lomi Bedo anayekuwa Naibu Spika wakati Baraza la Shirikisho limemchagua kiongozi wa zamani wa Mkoa wa Amhara, Agegnew Teshager kuwa spika wa baraza na Zehara Oumed kama naibu spika.
 
Siku za hivi karibuni imekuwa ni fahari au kawaida kwa watu wengi kuishi pamoja na mbwa au paka ndani ya nyumba zao.

Tunaweza kusema ni usasa, kwani wakati mwingine, mbwa hao wamekuwa wakibebwa na kubembelezwa mithili ya binadamu, wakati mwingine hata kulala kitandani katika viti na wengine kupewa mahitaji yote ya kibinadamu.

Hapa nchini hili limeonekana kufanywa zaidi na mstaa wa tasnia ya burudani.

Baadhi wamekuwa wakiambatana na mbwa hao kila sehemu wanayokwenda, kuwabeba mikononi na kuwabusu pale wanapoona inastahili.

Kituo cha Udhibiti wa magonjwa nchini Marekani ‘Center for Disease Control (CDC)’ kinaonyesha kuwa uwepo kwa mbwa hao katika nyumba husaidia kuwaondolea watu msongo wa mawazo, lakini pia kinatahadharisha uwezekano wa wamiliki kupata magonjwa kutoka kwa mbwa hao.

Hiyo ni kwa sababu mbwa hao wakati mwingine hubeba vijidudu au bakteria ambao husababisha maradhi. Magonjwa hayo wakati mwingine huwa madogo madogo na mengine makubwa.

Kwa mujibu wa CDC, yapo magonjwa, bakteria, minyoo, kupe na viroboti kwa ujumla wake takribani 17 anavyoweza kuambukizwa binadamu kutoka kwa mbwa.

Baadhi ya magonjwa ni kichaa cha mbwa ambacho hutokea mhusika anapong’atwa, lakini bakteria, minyoo na wadudu wengine humuathiri mtu bila kung’atwa.

Yapo magonjwa mengine ambayo binadamu huweza kuyapata kwa kumgusa au kumshika mbwa aliyeathiriwa na ugonjwa huo.
 
Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema kumekuwa na ongezeko la malalamiko ambapo mwaka 2020 yalikuwa 1,197, lakini katika kipindi cha Julai hadi Septemba, wamepokea malalamiko 170.

Imebainishwa kuwa kati ya hayo, 130 ni ya kelele na mitetemo, huku baa na kumbi za starehe yakiwa malalamiko 60.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Meneja wa NEMC Kanda ya Morogoro-Rufiji, Amina Kibola wakati akielezea hali ya uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemo, katika warsha iliyowakutanisha NEMC na wamiliki wa kumbi za starehe, bendi, baa na wadau wa muziki.

Alisema malalamiko mengine yalihusu viwanda, matangazo, nyumba za ibada, mashine za tofali na vyombo vya moto.
 
Aisee
 
Jordan Pickford ambaye ni Golikipa wa Everton aliwahi kupingwa sana kutokana na kimo chake, wanasema ni mfupi hivyo ni ngumu kuwa Kipa bora

Miaka inazidi kwenda anazidi kuwa tegemeo Everton na England kwa ujumla
 
Uza vile vi umbwa vyako. Shauriro Tojo
 
Kinachoisaidia Mbeya Kwanza ni ile morali ambayo wametokanayo Ligi Daraja la Kwanza na muda ambao wamepata kwa ajili ya maandalizi.

Ukiangalia kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City walishatanguliwa kwa magoli mawili lakini wakarudi. Kama wachezaji hawapo vizuri kichwani na kimwili ni vigumu sana kurudi.

Inaonekana mwalimu wa Mbeya Kwanza alifanyia kazi vizuri fitness ya wachezaji wake kwa sababu wako fit kupambana muda wote lakini pia ametengeneza saikolojia kwa sababu wachezaji wana ari.

Mbeya Kwanza wanaamini kwenye ligi hawajaja kusindikiza na hawajapanda kwa kubahatisha.

- Amri Kiemba.
 
Msimu uliopita Azam FC ilianza vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara ukilinganisha na msimu huu, msimu uliopita walishinda mechi sita mfululizo!

Msimu huu baada mechi mbili Azam imepata pointi moja tu! Imetoka sare na Coastal Union na kupoteza kwa Polisi Tanzania.

Azam ilianzia Mkwakwani uwanja ambao haijapata ushindi kwenye mechi tano za hivi karibuni! Halafu ikakutana na Polisi Tanzania timu ambayo imesajili wachezaji wengi msimu huu lakini inaonekana si tatizo kwao.

Azam inawakosa wachezaji wake waandamizi kikosini [Aggrey Morris, Sure Boy na Mudathir Yahya] ambao inaelezwa wamesimamishwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…