"Askari hawa Waliopambana na Hamza miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa"
"Polisi walipambana kuhakikisha kwamba madhara makubwa zaidi ya yale yaliyotokea hayatokei, nani ambaye hafahamu kama yule Mhalifu (Hamza) angeondoka na zile silaha zilizokuwa na magazine mbili na risasi 60 na nyingine alizokuwa nazo nini kingefanyika"
"Kazi ya Polisi ni kulinda Watu na mali zao, ukielewa sehemu moja Watu wanapiga risasi ukaamua kufa kwa ajili ya Watu wengine sio kazi ya kubeza, kazi ya Upolisi sio kazi ya kuitafsiri kirahisi kama baadhi ya Watu wanavyofanya"
"Niendelee kuwatia moyo Askari waliojeruhiwa katika tukio la mapambano kati ya Polisi na Hamza na niendelee kuzitia moyo Familia zilizopoteza Wapendwa wao"------Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro