Wakati Serikali ikitoa takwimu za waliopata chanjo ya Uviko-19 kuwa 207,391, baadhi ya watu ambao hawajachanjwa katika nchi kadhaa duniani wameanza kukosa huduma mbalimbali.
Miongoni mwa huduma hizo ni safari za kimataifa, kazi, utoaji huduma katika migahawa, hospitali, masoko ya ndani ‘supermakert’.
Machi mwaka huu, Saudi Arabia ilitangaza kuwa waumini wa dini ya Kiislamu watakaoruhusiwa kuhudhuria ibada ya Hijja kwa mwaka 2021 wanapaswa kuthibitisha kuwa wamepatiwa chanjo dhidi ya Uviko-19.
Tayari nchi 27 zinazounda Jumuiya ya Ulaya zimeshakubaliana pasi na chanjo mtu hatoruhusiwa kuingia kwa nchi mwanachama.
Kwa nchi za Afrika Mashariki Kenya, Rwanda na Uganda kila moja imetoa masharti kwa wafanyakazi wawe mapata chanjo hiyo ndipo waruhusiwe kuendelea na kazi.