Ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu leo Dar es salaam kwenye kongamano la mwaka mmoja toka kifo cha Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa lililoandaliwa na
Pamoja na mambo mengine aliyoyaongea Rais Samia kuhusu Hayati Benjamin Mkapa, ametilia mkazo umuhimu wa Watu kuendelea kujikinga dhidi ya corona na kusisitiza pia kwamba chanjo Nchini Tanzania halitokua swala la lazima.
“Serikali inaendelea kumtaka kila Mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona, tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huu ambapo kwa sasa tunakamilisha taratibu za kuagiza chanjo kwa ajili ya kinga, mwelekeo ni kwamba kila atakayehitaji huduma ya chanjo iwe inapatikana na chanjo hiyo ni ya hiari” ——— Rais Samia.
View attachment 1853675