At least hapo nawaona Garda world ambao ni private zamani Ultimate...Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipa siku saba za awali Tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko la kimataifa la Kariakoo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 11, 2021 alipokuwa anaongea na Wafanyabiashara na Wakazi wa eneo la Kariakoo baada ya kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto huo, Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, TAKUKURU, TANESCO, Wakala wa Majengo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na DPP.
“Endapo itagundulika kama kuna Mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, hatua kali za kisheria zitachukuliwa moja kwa moja, kitendo cha kuungua kwa soko hili la miaka chungu mzima lazima kuwe na uchunguzi wa kina, kwanini leo lishike moto”———-MajaliwaView attachment 1849512View attachment 1849513View attachment 1849514
Anaacha ku deal na waandamaji wa Zuma wanaoiba kwenye maduka, anahangaika na lockdown...Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameongeza wiki mbili nyingine za “lockdown” kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya Covid- 19 nchini humo.
Hatua hiyo imekuja kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Afrika ya Kusini.
Ramaphosa alisema kuwa shule zitaendelea kufungwa na kuendelea kuzuia mikusanyiko katika sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe.
Huku sehemu za mazoezi na migahawa katika sehemu mbalimbali ya miji ikiruhusiwa kufunguliwa kwa sharti la wateja wao kukaa mbalimbali.
“Serikali itaongeza fedha katika mfuko wa Covid ili kufidia biashara zilizoathiriwa,” Rais alisema.
Afrika Kusini imeripoti maambukizi mapya 16,302 siku ya Jumapili yakileta jumla ya idadi ya maambukizi kuwa 2,195,599.
Jana watu 151 walifariki kwa sababu ya Covid na kusababisha idadi ya vifo kufikia 64,289View attachment 1850488
Machinja complex hoyeee...Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameruhusu kuanza kwa shughuli za biashara Kwenye soko dogo la Kariakoo Kutokana na eneo hilo kutoathiriwa na moto.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea sokoni hapo ambapo ametaka Wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara zao eneo la hifadhi ya Barabara ya kuingia sokoni humo waondoke ili Barabara ibaki wazi.
Makalla amesema kwa wakati huu ambao hali ya usalama soko kubwa haijakaa sawa anashauri Wafanyabiashara wachukue mali zao na kuhamia Soko la Kisutu na Machinga Complex hadi marekebisho yatakapofanyika.
Kuhusu Soko la Shimoni ambalo inaelezwa halijaathiriwa kwa kiasi kikubwa na moto, RC Makalla amesema Kutokana na mfumo wa umeme sokoni humo kuharibika ameagiza ufanyike uratibu Wafanyabiashara wakachukue bidhaa zao na kuhamia Soko la Machinga Complex na Kisutu.View attachment 1850701