Makapuku Forum

Ujasiri, uzoefu na kutokuhaha ni miongoni mwa vilivyosaidia kuishusha salama Ndege hii ndogo na kutua nayo kwenye barabara kuu baada ya kukosa nguvu ikiwa angani huko Agoura California Marekani.

Ndege hii ilikua na Mwanafunzi wa Urubani na Instructor ambao walikuwa na dakika 6 tu za kutafuta sehemu ya kutua baada ya kugundua Ndege hiyo aina ya Cessna 172 tatizo.

Mwalimu wa Urubani aliyekuwemo kwenye Ndege hiyo Captain Trevor Peterson ambae pia ni Mwanajeshi wa Marekani ilibidi alimuweka pembeni Mwanafunzi na kuishusha Ndege salama.
 
Polisi Mkoani Iringa wamewakamata Wahamiaji 62 wasio na vibali ambao ni Raia wa Ethiopia waliokuwa wakisafirishwa kutoka Morogoro kuelekea Mbeya na kisha Afrika Kusini, walikuwa wamepakiwa kwenye lori aina ya Scania.
 
Rais Samia Suluhu leo amepokea mapendekezo ya mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na Corona na mapendekezo ya mpango kazi wa uratibu wa utoaji chanjo ya Corona yaliyowasilishwa na Kamati aliyoiunda kuishauri Serikali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Said Aboud aliyeongozana na Mwenyekiti wa Kamati, swipe kuisoma taarifa yote.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…