Mbunge wa Muheza Tanga ambae pia ni Msanii, Hamisi Mwinjuma MwanaFA amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kanuni iliyoanza kutumika na BASATA ya kukagua nyimbo za Wasanii wote Tanzania kabla ya kupelekwa Redioni.
Kupitia XXL ya Clouds fm amesema ———> "Sidhani kama muziki unahitaji mipaka mingi kiasi hicho japokua siungi mkono kuwa na lugha chafu au maneno ya matusi kwenye nyimbo sababu muziki unasikika sana na tunaharibu hata Watoto mapema na kutengeneza matabaka flani nyimbo haziwezi kusikilizwa ukiwa na Mtu flani"
"Niliuliza hili swala kwenye group la Whatsapp wakasema wanataka kutumia software kufanya shughuli hii mimi nikauliza kama BASATA wanaweza kutumia software kufanya shughuli hii software haiwezi kujua mafumbo na Watu wakitumia mafumbo kwahiyo kama ni bora wasitumie kitu waziache nyimbo ambazo hazina matusi ya moja kwa moja zipigwe tu Redioni"
"Hii sheria ya kimsingi ya kupitisha nyimbo BASATA zikasikilizwe kwanza kabla ya kupelekwa Redioni sifikiri kama ina msingi wowote lakini sheria ni sheria acha tuiangalie huku tuongee na Watu wa Wizara, tuongee na Waziri, Katibu Mkuu kuona namna marekebisho yanaweza kuja ya sheria ili mradi iondoke na iache muziki huru, kimsingi mimi siko nayo na naamini haki itatendeka na haitoendelea kutumika kuwabana Wasanii na kuurudisha muziki nyuma" ———