Makapuku Forum

Mwili wa Hayati Dkt.Magufuli unatoka Ikulu saa 2:30 asubuhi hii kwenda Kanisani St Peters kwa ajili ya Ibada na kisha saa 3:00 asubuhi utapelekwa Uwanja wa Uhuru, hizi picha ni kutoka Uwanja wa Uhuru za maandalizi ya utakapoagwa mwili. RIPHayatiMagufuli
 
Kutokea Kanisa la St.Peters Dar es salaam, mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dr.John Pombe Magufuli tayari umefikishwa kwa ajili ya Ibada kabla ya kupelekwa Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuagwa.
 
Kutokea Kanisa la St.Peters Dar es salaam, mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dr.John Pombe Magufuli tayari umefikishwa kwa ajili ya Ibada kabla ya kupelekwa Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuagwa.
RIPHayatiMagufuli
 
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ulivyotolewa katika Kanisa la St. Peter’s baada ya Ibada kukamilika, tayari kuelekea Uwanja wa Uhuru.
RIPHayatiMagufuli
 
Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwl. Nyerere, Mama Maria Nyerere akiingia kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuuaga mwili wa Hayati Magufuli.
RIPHayatiMagufuli
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume akiingia kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kumuaga Hayati Magufuli.
RIPHayatiMagufuli
 
Viongozi mbalimbali wa Vyama Vya Siasa, Dini na Serikali wakiingia Uwanja wa uhuru muda huu kwa ajili ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli, kwenye hizi picha kuna Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Askofu Ruwaichi, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, RC Kunenge na Viongozi wengine.
RIPHayatiMagufuli
 
Hizi ni picha nyingine kutoka Kanisa la St Peter’s Dar es salaam mapema leo wakati wa Ibada kabla ya kupelekwa Uwanja wa Uhuru.
RIPHayatiMagufuli
 
Wananchi wakiwa wamejitokeza Barabarani kuuaga mwili wa Hayati Magufuli wakati ukiwa unapelekwa Uwanja wa Uhuru huku wengine wakiutandikia msafara kanga ili upite juu yake.
(
via TBC)
RIPHayatiMagufuli
 

Attachments

  • 20210320_130107.jpg
    47.5 KB · Views: 3

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…