Makapuku Forum

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Chilo (wa pili kulia) akiwaongoza Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi vilivyopo chini ya Wizara hiyo kula chakula kinacholiwa na Wafungwa katika Gereza la Wilaya ya Singida ambapo baada ya chakula hicho alipata nafasi ya kuzungumza na Wafungwa.
 
Juzi kwenye moja ya Habari kubwa za Kitaifa tulizokua nazo ni kukamilika kwa asilimia 100 kwa Stesheni ya Dar es salaam ya reli ya kisasa (SGR) ambapo baada ya ujenzi kukamilika kwa 100%, samani za kisasa zimeanza kuwekwa ndani yake kama meza, viti na makochi tayari kabisa kwa kuanza kazi, hizi ni picha za juu za Stesheni hiyo.
 
Serikali imepongezwa kwa kutenga Tsh. Bilioni 15.5 kwa ajili ya uwekezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha kufanya vipimo vya Saratani kwa kutumia teknolojia ya nyuklia (PET CT Scan) pamoja na kiwanda cha kuzalisha mionzi dawa (Radio Isotopes).

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo, wakati kamati hiyo ilipotembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), iliyopo Dar es Salaam.

Nyongo amesema Serikali imeipa kipaumbele Sekta ya Afya, uwekezaji wa mradi huo utakuwa ni wa kihistoria, wa kimkakati na kwamba utaiweka Tanzania kwenye dira ya Kimataifa kwenye eneo la afya na kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia Watanzania na hata Wageni kutoka nje ya Nchi kupata matibabu sahihi na kwa wakati ya Saratani.

"Hatua hii ni kubwa, mradi huu itasaidia Watu wengi kupata huduma hizi za kibingwa kwa wakati kwani Watu wengi walikuwa wanafika kupata huduma wakiwa Kwenye hatua za mwisho”
 
Serikali imesema itatatua changamoto ya vifaa katika Sekta ya Filamu kwa kuanzisha maktaba itakayokuwa na vifaa vya aina mbalimbali vitakavyotumika katika Tasnia hiyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa alipokutana na Waigizaji wa Tamthilia ya Tunu katika Hospitali ya Kairuki DSM.

"Serikali na Watanzania tupo pamoja na nyinyi na tunawakubali sana Waigizaji wetu na vipaji mlivyonavyo, tumejipanga kuwasaidia kutengeneza Filamu bora ili Watanzania wanaoutuunga mkono waendelee kuburudika kwa Filamu nzuri”- BASHUNGWA

"Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha ajira Milioni 8 ambazo tumeahidi kwenye Ilani ya CCM, Tasnia ya Sanaa na Michezo tutatoa mchango mkubwa na tutafanya hivi kwa kushughulika kwa changamoto ambazo mnakabiliana nazo ikiwemo vifaa ambapo tuna mpango wa kujenga maktaba ya vifaa ili Maproducer, Waigizaji wawe wanachukua kwa utaratibu kama ilivyo Maktaba za Vitabu”
 
“Nimekuja hapa (Tanga) niwasalimie lakini kubwa niwape salamu za Rais, Rais anawasalimia sana na anawashukuru sana kwa kazi nzuri mliyofanya mwaka jana kurudisha Serikali ya CCM madarakani, Rais anasema tupo salama, tuchape kazi, twende vizuri,tujenge upendo na mshikamano wa Watanzania ili Taifa letu likuwe liwe na tija zaidi”———>Mama Samia Suluhu, Makamu wa Rais wa Tanzania akiwa kwenye ziara Mkoani Tanga leo
 
“Katika wakati muhimu wa Watanzania kushikamana ni wakati huu, wakati wa kujenga umoja ni huu, sio wakati wa kusikiliza maneno ya kutoka nje yakatuparaganisha, tuchape kazi, tujenge umoja ili Tanzania iwe Taifa imara”-Mama Samia Suluhu, Makamu wa Rais wa Tanzania akiwa ziarani Tanga

“Niwahakikishie Wananchi, Tanzania tuko salama, chapeni kazi ili kuleta maendeleo, uimara wa Taifa letu unaleta maneno mengi, msibabaishwe na maneno ya Watu walioko nje”———>Mama Samia
 
Polisi Mkoani Kilimanjaro wanawashikilia Watu wawili ambao ni Peter Silayo na Melchiory Shayo, kwa tuhuma za kusambaza mitandaoni kwamba Wakuu wa Serikali ni wagonjwa, Kaimu RPC Kilimanjaro Ronald Makona amewataka Wananchi kuacha kusambaza taarifa zinazoweza kuzua taharuki na kwamba watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limethibitisha kuwa linamshikilishia Tito Augustino Kiliwa Mkazi wa Mufindi kwa kosa la Kuchapisha kwenye Mtandao wa Facebook taarifa za uzushi kuwa Rais Magufuli anaumwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Rienada Millanzi amesema March 11,2021, kupitia ukurasa wa Facebook, Mtuhumiwa aliandika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaumwa, ujumbe ambao ulileta taharuki ndani ya Jamii.

“Unapozungumzia Kiongozi wa Nchi anaumwa wakati wewe sio mtoa taarifa katika ngazi hiyo hilo ni Kosa lazima tuchukue hatua na baada ya kumfikisha Mahakamni sheria itafuata mkondo wake”- Kaimu RPC Iringa

Mtuhumiwa amekamatwa kupitia kikosi maalum kinachoshughulika na makosa ya mtandao na atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
 
Madereva wa Daladala Jijini Mbeya wamefanya mgomo leo wenye lengo la kuishinikiza Serikali kuziondoa Bajaji katika Barabara zilizoainishwa kuwa ni maalum kwa matumizi ya Daladala.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Denis Daudi amesema tayari wanazo taarifa hizo za mgomo na wanapambana ili kumaliza mgogoro huo.

Kwa sasa Madereva Bodaboda wameendelea kutumia fursa hiyo kusafirisha Abiria huku bei kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiongezwa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…