Ukweli huu taratiibu nahisi unayabadilisha maisha yangu kwa jinsi ambavyo nawatazama wengine.
Ni kwamba maisha ni kama movie na kila mmoja ni director wa movie ya maisha yake, wengine wote ndugu, marafiki na wapenzi ni wahusika ambao wanakamilisha movie hiyo.
Kila mmoja amempangia nafasi fulani katika hiyo movie yake. Hatarajii uzidishe au upunguze majukumu yako aliokupangia katika hiyo movie yake.
Sababu zinazopelekeaga tunaumia kutokana na matendo ya wengine ni pale tunapozidisha au kupunguza majukumu waliotupangia katika movie zao.
Tambua nafasi yako, fanya kama mwenye movie anavyotaka ufanye. Hii itakupunguzia stress zisizo za lazima katika maisha yako
SAVE hii ikukumbushe kila unapokua na stress zinazo sababishwa na wengine.