Makapuku Forum

Makapuku Forum

..
Screenshot_20190507-162315.jpg
 
"Wakati tunaanza tulikuwa tunafanya Muziki for love, lakini Clouds Fm walipokuja walibadilisha system na kuufanya Muziki wa nyumbani uanze kutengeneza pesa nyingi sana.
-
"Sababu kwa kipindi hicho FM stations nyingi zilikuwa zinapiga Muziki wa nje, Clouds walikuja na plan yao nyingine ili kutoboa. Nakumbuka Kusaga na Ruge walitufuata studio zote zinazofanya Music Productions na kutusihi kutoa nyimbo katika Digital Format.
-
"Walisema wao kama wao watahakikisha kuwa Wana Push sana lakini tuhakikishe ubora upo vizuri na ndipo hapo vipindi kama Afrika Bambataa vikazaliwa n.k.
-
"Wakati tunaanza kwa wimbo mmoja tulikuwa tunafanya 5,000/= kuna msanii mmoja akanambia yeye atakuwa ananipa 10,000 kwa kila wimbo.
-
"Nilifanya nae Albamu yenye nyimbo 10, baada ya kusaini mkataba na msambazaji alipewa milioni kadhaa, alikuja akanipa laki moja nakumbuka pesa yote hiyo nilienda kuimalizia disco ya Kusaga huko Tazara, Pombe na Warembo wa kutosha yote ikaisha.
-
"Shoo moja kali kwa msanii akiitwa alikuwa analipwa laki moja, lakini kulikuwa na hela sana kuna muda upo unakamilisha Albamu msambazaji anatoa Advance ya mwanzo kabisa Milioni 100.
-
" Wasanii wengi sana wamekula pesa mfano kama Wagosi Wa Kaya hao wamekula sana hela tena sana, sababu mimi nikipiga hesabu kwa pesa niliyokula kupitia wao ni nyingi sana je vipi kwa wao?.
-
"Niliwashauri wajenge nyumba sababu upepo wa Muziki muda wowote unabadilika, lakini niwe mkweli hawakujenga kuna siku waliniuliza Masta Jay hiyo BMW yako sh ngapi? Nilipowatajia kesho walikuja na pesa wakachukua funguo.
-
"Wasanii wa zamani walichokuwa wanawaza ni kupendeza, mademu na pamba tu lakini kufanya mambo mengine ya umuhimu ilikuwa ni tatizo sana.
-
Dondoo Ya Vitu Muhimu Alivyoongea Master Jay' Katika Interview na Clouds Fm Wiki 2 Zilizopita.
Screenshot_20190507-162613.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom