Makapuku Forum

Makapuku Forum

.
Screenshot_20181109-073908.jpeg
 
Unaona hicho kidoti. Hapo ni nyumbani. Hicho kidoti ni sisi. Ndani ya hicho kidoti kila mtu unayempenda, kila unayemfahamu, kila uliyewahi kumsikia, kila mwanadamu aliyewahi kuishi.

Furaha zetu na mateso yetu, Dini zote, itikadi za watu mbali mbali, nyanja za uchumi, kila muwindaji na mtafutaji, kila shujaa na mwoga, kila mtengenezaji na muhalibifu wa mazingira, kila mfalme na mkulima, vijana wote waliokuwa kwenye mahusiano, kila mama na baba, watoto, wagunduzi, wavumbuzi, kila mwalimu wa maadili, kila mwanasiasa mla rushwa, kila mtu maarufu, kila mtawala, kila mtakatifu na mtenda dhambi katika historia ya maisha yote ya binadamu wote wameishi kwenye hicho kipunje kidogo kinachoonekana kwenye muale wa Jua hapo.

Dunia ndiyo sayari pekee kwa sasa ambayo viumbe hai wanaweza kuishi. Hakuna mahali pengine kama hapa Duniani. Sayari yetu hii iko peke yake kwenye huu ulimwengu mpana usiokuwa na kikomo na hakuna dalili yoyote inayoonesha kuna kitu kitakuja kutusaidia kwenye matatizo yetu yanayosababishwa na chuki zetu wanadamu hapa Duniani.

Kwangu mimi hii picha inayoonesha punje ya kiulimwengu chetu kidogo (Dunia) wanadamu tunajukumu la kupendana sisi kwa sisi, na kuhakikisha tunakipenda na kukitunza hiki kidoti cha bluu ambacho ndani yake tunaishi sisi binadamu, au makazi pekee ambayo tunayafahamu. - Carl Sagan, 1990

Maneno hayo yalizungumzwa na Carl Sagan Tarehe 14, mwezi wa pili mwaka 1990, baada ya kuoneshwa picha hii inayofahamika kama "Pale Blue Dot" ambayo ilipigwa na chombo kinachoitwa Voyager 1 wakati kikiwa kinatoka kwenye mfumo wetu wa Jua na kuingia kwenye anga la ndani zaidi
Screenshot_20181109-074840.jpeg
 
Wanawake wanaovuta sigara, wanaougua kisukari au waliyo na tatizo la shinikizo la damu wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo.

Kwa mujibu wa utafiti mpya uliyofanywa nchini Uingereza, wananawake wanastahili kupewa ushauri sawa na wanaume na pia kupewa ushauri wa kuachana na uvutaji sigara.
Screenshot_20181109-075210.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom