Makapuku Forum

TUOMBE:Baba Mtakatifu Mungu wetu mwenye upendo mkuu Asante sana kutuamsha salama leo Jumamosi tarehe 27 Oktoba 2018 tukiwa wenye Afya njema .Wapo wengi walitamani kuiona leo Hawajaweza.. Tunawaombea wote waliopoteza ndugu,jamaa ,marafiki wenza wapate faraja kuu tunawaombea wajane,wagane yatima wapate tumaini na kukutegemea wewe tu Baba wa ya yatima.Tunaomba Amani itawale.Tunajikabidhi leo hii mikononi mwako kaa nasi Baba ongoza ratiba zetu zote uwe nasi katika Majonzi ,katika furaha,katika kazi hesabu hatua zetu tukutangulize katika kila jambo Mfalme wa Amani.Uwe Tumaini letu katika yote .Tujalie safari njema majini ,nchi kavu,angani tuende na kurudi salama..Tunaomba bariki kazi za mikono yetu tusaidie tupate yote ambayo umetujalia.Mungu wetu tunawaombea watoto na wajukuu zetu wawe salama popote walipo...Wasaidie watoto wetu wakujue na wakufuate wewe katika maisha wakutegemee katika kila jambo.Tunaomba Amani Mshikamano, kuvumiliana na Upendo wako utawale.Ponya wagonjwa na wote wanaopitia changamoto mbalimbali na watu wote wapate haja za mioyo sawasawa na mapenzi yako.Roho Mtakatifu kaa nasi .
Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen.
JUMAMOSI NJEMA YA BARAKA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 
Tabasamu la kila mmoja kati yetu hutegemea usafi wa kinywa chake unaotokana na kupiga mswaki na kusugua kwa umakini. Changamoto iliyopo ni namna ya kufanya hivyo kwa ufasaha.

Wengi hawafahamu njia sahihi za kupiga mswaki kwa ajili ya afya ya kudumu ya kinywa inayoaanza hapo. Kinywa safi ni msingi wa afya njema ya mwili.

Afya ya kinywa inaanza na meno yaliyo safi. Hili hufanyika kwa kutunza maeneo na meno yanakutana na fizi katika hali ya usafi huzuia magonjwa ya fizi na kuzuia kutoboka kwa meno.

Kufanikisha usafi wa kinywa na meno, kila mmoja anapaswa kuzingatia upigaji sahihi wa mswaki kila siku au inapohitajika. Yapo mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kupiga mswaki lakini nitaeleza matano kwa leo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…