Chelsea iko tayari kutumia Euro milioni 20 (£17.6m) kumpata kiungo wa kati wa Brescia mataliano Sandro Tonali, 28, katika dirisha la uhamisho. (Calciomercato)
Southampton, Crystal Palace na Cardiff wanamfuatilia mshambuliaji wa Roma mzaliwa wa Bosnia Edin Dzeko, 32, ambaye anataka kurudi katika ligi kuu ya England. (Mirror)
Winga wa Ubelgiji Kevin Mirallas, 31, hana mpango wa kurejea Everton kibarua chake cha kuchezea Fiorentina kwa mkopo kitakapo malizika. (La Nazione - in Italian)
Mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny, 33, amesema alikuwa anashabikia Croatia kisiri dhidi ya taifa lake Ufaransa katika fainali ya kombe la Dunia baada ya kuachwa nje ya kikosi hicho kutokana na jeraha. (Canal Plus, via Goal.com)
Messi anaweza kuondoka Barcelona mwaka 2020 lakini mkataba wake unaeleza kuwa kama ataondoka basi hataruhusiwa kujiunga na timu nyingine "kubwa". (Mundo Deportivo)