Tembo ni mnyama aishie mbugani, ndio mnyama pekee ambaye ni mkubwa kuliko wanyama wote katika uso wa dunia, mnyama huyu ni mrefu pia mnene, ana wastani wa kilo zaidi ya elfu saba, kwa lugha nyepesi namaanisha tani saba, mbali na uzito huo lakini ana urefu wa futi kumi na tatu ni kimo kikubwa sana, miguu yake ya mbele ni mirefu kidogo kwa miguu ya nyuma, mnyama huyu hula majani, mizizi, matunda nk, chakula chake hutokana na mimea tuu.
Kichwani kwake ana viungo vyote alivyo mwanadamu, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya viuongo vyake huwa havionekani kwa urahisi, mfano watu wengi huwa hawajui mdomo wa tembo upo eneo gani ! na wanaoweza kukuonesha mdomo wanaweza shindwa kabisa kuonesha pua ya tembo ilipo, masikio yake ni makubwa sana ukiyafanya sahani unaweza kuweka msosi hata wa watu kumi, kama wakila pamoja.
Tembo ndio mnyama pia ambaye ana kichwa kikubwa, ambapo ndani ya kichwa chake kuna sehemu kubwa iliyobeba ubongo wake, Tembo wa Africa ndio tembo wakubwa na wenye mvuto sana, hubeba mimba kwa miezi 22 yaani mwaka mmoja na miezi kumi, baada ya hapo huzaa mtoto mmoja au wawili, watoto wa tembo huzaliwa wakiwa na kilo zaidi ya 100.