Makapuku Forum

Wanawake mbioni kupatiwa emoji ya hedhi ambayo itakuwa inatumika kama njia mbadala ya mawasiliano kwenye simu kuonesha kipindi wanacho kipitia pasipo kujisikia vibaya, pia kuondoa aibu pale mwanamke anapotaka kuelezea hali yake kwa mtu mwingine kupitia emoji.

Mpaka sasa Unicode Consortium, taasisi isiyo ya kifedha inayomiliki emoji zote Duniani, bado wapo katika mchakato wa kutafuta emoji itakayofaa kutumika kama alama ya hedhi kwa mwanamke ila upo uwezekano mkubwa emoji yenye uso wa kutabasamu pamoja na tone la damu ndiyo itakayochaguliwa mwaka 2019
 
Kampuni ya Amazon wazidi kuongeza maduka ya Amazon Go, maduka ya bidhaa yasiyokuwa na wahudumu ndani, yaani duka halina mtu wa kukuhudumia badala yake unaingia unachukua bidhaa unayotaka kisha unatambaza alama za QR kwenye programu tumishi ya Amazon Go ambayo inakuwa kwenye simu yako.

Maduka hayo ya Amazon Go yanatumia kompyuta zenye uweledi wa hali ya juu pamoja na baadhi ya kamera zilizofungwa ndani humo kuweza kuangalia aina ya bidhaa mteja aliyochukua kisha kuhifadhi taarifa zake kwenye programu tumishi ya Amazon Go, programu ambayo ni lazima uwe nayo kwenye simu yako kama unataka kununua bidhaa kwenye maduka hayo yasiyokuwa na wahudumu ndani.

 
Kwa jina anafahamika kama John McaAfee ni mtaalamu wa masuala ya ulinzi wa programu za kompyuta, hivi karibuni aliweka dau la dola 250,000 (zaidi ya shilingi milioni 500 za kitanzania) kwa mtu yoyote atakayeweza kudukua pochi maizi (digital wallet) ya fedha za kidigitali Bitcoin, ikiwa ni sehemu ya kutangaza pochi mpya zinazotengenezwa na kampuni yake inayofahamika kama Bitfi ambazo wao wanadai haziwezi dukuliwa kwa urahisi.

Ila jambo la kushangaza pochi hiyo ili dukuliwa wiki chache zilizopita na kupelekea kampuni ya Bitfi kuondoa madai ya kutoweza kudukuliwa "unhackable" kwenye pochi hizo.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo John McAfee ambaye ndiye alikuwa kidedea katika kutangaza pochi hizo mtandaoni alisema wadukuzi hao ni waongo na hakuna hata mmoja ambaye alilipwa pesa ambazo ziliwekwa kwa mtu ambaye angeweza fanikisha kudukua pochi hizo.

McAfee pia alisema kama kweli kuna mtu anaweza kudukua pochi hizo na anajiamini, basi yeye yupo tayari kumlipia nauli ya ndege mpaka Marekani kisha ampatie moja kati ya pochi yake maizi (digital wallet) ambayo ndani ina Bitcoin zenye thamani ya dola milioni 20 (zaidi ya shilingi bilioni 45 za kitanzania) kama akiweza kuidukua basi anachukua hizo pesa.
 
Amen
 
Kweliii kabisa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…