
TUOMBE:
Mtakatifu,
Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi asante kwa siku ya leo JUMAMOSI Tarehe 25 Agosti 2018.
Tunakushukuru kwa neema hii ya uzima na huruma yako juu yetu ..
Asante kwa wema na fadhili zako umetutunza umetuponya na kutulinda siku zote umemimina Roho wako juu yetu matendo makuu Baba tumeyaona wiki nzima .
Tunaomba Toba kwa makosa yote tuliyotenda kwa kujua au kutojua..kwa mawazo ,maneno, matendo Uturehemu twakusihi nasi tunawasamehe wote waliotukosea walioomba msamaha na hata wasioomba.
Siku ya leo endelea kutupigania Baba angalia njia zetu zote Baba imarisha mahusiano yetu,Familia zetu,Watoto na Wajukuu wetu ,ndugu ,jamaa na marafiki zetu wakuone wewe.
Asante kwa ajili ya wenza wetu waimarishe kimwili na kiroho wapiganie Baba na wakuone wewe katika kila wanalopitia.
Tunakabidhi Roho zetu na miili yetu kwako tuweze kukutumikia.
Tunawakabidhi watoto wetu na wajukuu wetu zawadi kubwa uliyotupa Baba waimarishe na wafanikiwe Afya zao ziwe njema na wakusifu wewe kwa kila jambo.
Bariki kazi za mikono yetu.
Walinde wasafiri waende na kurudi salama Nchi kavu,Majini,Angani na kwa miguu .
Endelea kuwasaidia wajane,wagane,yatima na wanaopitia changamoto mbalimbali.
Tunamkataa shetani na kazi zake zote..Ashindwe katika jina la Yesu Kristo.
Karibu Roho Mtakatifu Kaa nasi Tuongoze.
Tunaomba na kuamini katika jina la Yesu Kristo Amen.
JUMAMOSI NJEMA YA BARAKA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE

