Makapuku Forum

Muziki: Sijachelewa

...natumaini ulikuwa na wikend njema Kapuku mwenzangu, upande wangu ilikuwa poa sana full kuogelea na nikwambie kitu, sikujua najua sana kupiga mbizi hadi nilipotupia zile bia za wasio raia (polisi) safari lager. Nilijiona napiga mbizi za kufa mtu na nisikuchoshe kwa kukuelezea wikend yangu ilivyokuwa maana yako hujataka kuisema, unaificha kama mtu aliyekula makande ya mbaazi. Nakusalimia mdau na kukuambia kuwa bila wewe jukwaa hili halina nguvu yoyote. Nimekuona moudgulf wikend ukapotea tena.

Muziki sasa, sijachelewa kama nilivyosema, nilikuwa nakuja ila njiani nikakutana na ahadi yangu moja ikabidi nikaitimize fasta bila kuchelewa na wewe nisikucheleweshee burudani mwanzo wa juma hili tunaloamini litakuwa poa kabisa. Nakupenda mdau wa Makapuku na uwe na wakati mzuri


 
Woyooooooooooooooo binamu asante
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…