Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Ujinga wa Maendeleo ya Vitu Bila Watu

Ni wiki nyingine tena tunakutana hapa, kama umegundua kuna mabadiliko kidogo kwenye kipengele hiki, muda wa kukujia unabaki ule ule ila siku ndo zimebadilika. Kwa sasa kitakujia kila Jumatatu-Alhamini, Ijumaa hakitakuwepo hiini kutokana na saau zilizo ndani ya uwezo wangu. Tuongelee maendeleo sasa.

Maendeleo ni dhana pana sana, unaweza kusema tu maendeleo ni mabadiliko toka hali fulani kwenda hali nyingine na mara nyingi huwa n hali ya juu zaidi. MAbdiliko kurudi chini haya si maendeleo, ni maanguko na yana hasara nyingi kuliko faida. Tafasiri unavyoweza.

serikali ya awamu hii kamakuna kitu inaweza kupongezwa ni kuongelea na kuimba kila siku kuhusu maendeleo. Nyimbo hizi si mbaya kuzisikia kila siku, zinaleta matumaini kwa wengi na kushangilia bila kufikiri sawasawa ni aina ya ujinga mwingine ambao tumeshindwa kuondokana nao wengi wetu. Kiufupi tu hakuna maendeleo ya vitu yanayoweza kudumu kama watu hawajaendelezwa.Ndiyo maana Mwalimu JKN aliweka jitihada kwenye elimu, ndiyo hakufanikiwa kwa kila mtu lakini wengi walishindanishwa na kusoma. BMW alipokuja alisisitiza elimu, msmi huyu alijua na JMK aliujua umuhimu wa elimu, alitoa mikopo kwa wastahili wengi. elimu ndo maendeleo, vitu huisha na maarifa hudumu. Huhitaji kuwa msomi kulijua hili.

Nimalizie tu kwa kusema, kitendo cha awamu hii kuona maendeleo ya vitu ndo muhimu ni cha kipuuzi, ni cha watu wasioshughulisha bongo zao, wanapenda kuvaa nguo mpya ilihali ndani wana uvundo wa vitunguu swaumu na nguru. Maendeleo ya elimu hudumu, husimama na yana mwangwi mkubwa kuliko vitu, na kingine, aya maendeleo ya vitu yanayoshadadiwa yatasimamiwa na kina nani ikiwa elimu imewekwa daraja la nne. Tafasiri unavyoweza
 
Asante binamu
 
Muziki: Ramadhani Juma la Kati


Ninakusalimia wewe ndugu yangu unayelifanya jukwaa hili kuwa la kipekee kabisa, najua majukumu yanakutinga na unakuja humu kwa machale, hakuna ubaya, uzuri ni kuwa uwepo wako humu unafanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Asante SHIMBA YA BUYENZE , Tumosa , Shunie , husna muba , Madame S , Bitoz , shululu , Lyon Lee , mbalizi1 , mzeewakungoa , Mndali ndanyelakakomu , sweetlee , ABJ , moneytalk , demi , O'Brian , omarion5 , Da'Vinci , BlessedHope , Sakayo , Transcend , dumejeuri , Mkushi wa kusi , Tetramelyz , EMMYGUY , Valentina na wewe ambaye unanisoma muda huu.

Muziki sasa, nikutakie wiki njema na yenye tabasamu kila unapotoka na kurudi

 
Asante sana binamu
 
asante
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…