Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Kukomaa Si Kukakamaa

Siku zinakwenda kwa kasi, mambo mengi yanabadilika na mengine hayabadiliki, yako vile vile. Miaka nayo inasogea. Hili halina ubishi hata kidogo, maisha lazima yasonge, siku hazigandi alijiimbia Jide. Kasi ya maisha inatukimbiza na wakati mwingine tunajikuta tunatoka au kutaka kutoka nje ya mstari. Maisha yanakuwa ya gharama kila siku, changamoto lukuki, biashara haziuzi, kazi mishahara haikutani, na bado inabidi taifa liendelee, uzalishaji unazidiwa na kuzalishana na hapo bado unasikia ahadi za kipuuzi, ahadi zisizoangalia kesho na maendeleo ya watu na vitu. Tafasiri unavyoweza.

Leo nitakurudisha uangalie wewe kama wewe, jiangalie maana chanzo chochote cha mabadiliko ukiacha mabadiliko ya kiasili, ni wewe. Kukomaa ni ile hali ya kutokata tamaa katika unachofanya, unakifanya na kuendelea kukifanya na hata ukibadili basi ni kutokana na mazingira basi unakiboresha ili usikumbwe na kimbunga, huku ndiko kukomaa (persistence) na si kukakamaa/kudadamaa (kwa wale gender sensitive fellas). Ukikakamaa basi tegemea kuvunjika na hakuna anayependa kukuona ukivunjika maana ukivunjika kukuunganisha ni gharama kubwa sana.

Tafasiri unavyoweza inafunga siku ya leo na kukutakia wiki njema na wote wanaotarajia kufunga Ramadhani wiki hii basi tuwe na maandalizi mazuri.
 
Nakusalimia binamu pole na mambo yote
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…