Makapuku Forum

Makapuku Forum

giphy.gif
 
Tafasiri Unavyoweza: Hekima Tunu, Utawala Unapewa

Kiongozi mzuri ni yule anayeonesha njia na katika hali zote, za furaha au huzuni hawaachi wote anaowaongoza. Nimeanza na manenyo haya kwa sababu uongozi ni kuaminiwa. Ikitokea kila unalofanya unawafanya wengi wajihoji kama kweli unaaminika au unajifanyia kwa utashi wako peke yako kwa kuwa wewe ni kiongozi, basi inabidi urudi nyuma na ujitafakari. Tafasiri unavyoweza.

Tusidanganyane kuwa kila mmoja anaweza kuwa kiongozi, uongozi ni sayansi inayomfanya mmoja kujitambua kibinafsi (personal identit and self-awareness) na kutambua madhaifu yake na hivyo kutafuta suluhu ya kupunguza madhaifu binafsi (making accomodations for personal weakness). Udhaifu ni sifa ya kibinadamu, kila mmoja ana madhaifu yake lakini ukiwa kiongozi madhaifu haya hupaswi kuyatanguliza dhidi ya maslahi ya unaowaongoza.

Tabia kubwa ya kiongozi ambaye hawezi kudhibiti madhaifu yake ni kutaka kuhalalisha madhaifu yake kwa lugha za vitisho, kejeli na kujiamulia binafsi bila kushirikisha vyombo vingine ambavyo vinapaswa kumsaidia kuongoza. Tunashuhudia mengi sasa na kwa sababu ya hulka ya kiongozi tuliyenaye nyumbani inakuwa ni ngumu kuhoji kila anachofanya maana usifurahie sana kumuona kiongozi anayeambatana na jeshi/polisi kila anapotaka kukutana na wewe. Kesho ukimwambia unahitaji kuwa na hekima ataongoza na IGP, CDF na vifaru.
 
Muziki: Wiki Njema

Nilikuwa na weekend ya kipekee kidogo, mvua nyingi na hivyo nikashinda ndani ninafurahi na wote walio karibu yangu na hasa yule tunayekaribianaga sana faraghani. Msichezee mvua, zina mengi na zinakuhakikishia uwepo wa neema katika nchi. Ninakusalimia Kapuku na kukutakia week njema ambayo tayari umeshaianza.

Ni jambo zuri kuwaona wadau wote wakiwa wamekuja na kutoa HI jukwaani. Wengine tupo na tunafurahi wakati wote ukiwepo wewe unayenisoma muda huu.

Muziki sasa, anko wangu alikuwa busy kidogo na mambo ya uteuzi na japokuwa ahajaniambia uteuzi wake ulikuwa unahusu nini lakini kuna vitu vya kiasili ndo uteuzi wa anko wangu huwa unaangalia zaidi.

 
Back
Top Bottom