Makapuku Forum

Kazi yako ni njema mtaasisi
 
Muziki: It is Almost Furahiday


U khali gani Kapuku tunayeheshimiana, mimi sijambo na ninakusalimia kukukumbusha tu kuwa kesho ni Ijumaa, yaani Furahiday na wakati huu unapokuwa umeshajirejesha nyumbani baada ya kazi nimeona ni vizuri kukukumbusha.

Ninawasalimia wadau wote ambao huwa mnakuwa na muda wa kutembela hapa.

Muziki sasa, nikutakie wakati mzuri na maandalizi mema ya Ijumaa

 
Tuko pamoja mtaasisi
 
Muziki: Potea Njia

....ni wakati wa kwenda tu ndo unaweza kupotea njia lakini sio wakati wa kurudi. Ninakusalimia Kapuku mwenzangu na kukutakia wiki yenye mafanikio

Muziki sasa, burudika kufidia ukimya uliopo na unaotawala humu

 
Muziki: Potea Njia

....ni wakati wa kwenda tu ndo unaweza kupotea njia lakini sio wakati wa kurudi. Ninakusalimia Kapuku mwenzangu na kukutakia wiki yenye mafanikio

Muziki sasa, burudika kufidia ukimya uliopo na unaotawala humu

Binamu
 
Tafasiri Unavyoweza: Mkumbatie Simba Kwenye Picha

Zimepita siku kadhaa sijaandika kipengele hiki, kimahususikabisa ni siku mbili sijaandika kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Tafasiri unavyoweza. kuna mengi yamepita katika siku hizi ambazo sikuandika, mengi unayajua na mengine huyajui maana ni ngumu kujua kila kitu hata kama utakuwa unakaa jirani na radio au luninga. Mimi nayajua machache na ndiyo maana kuja kwangu hapa ni njia mojawapo ya kuongeza ufahamu maana wewe unayenisoma una mchango mkubwa katika kuifanya akili yangu kuwa 'sharp', asante sana kwa busara unazoleta hapa Makapuku forum.

Ukweli usemwe, kumekuwa kimya humu, sana tu tangu wiki ya Pasaka na unaweza kujiuliza mengi, ni muda au majukumu yamezidi. Kuzidi kwa majukumu si jambo baya, kadri unavyokuwa kiumri na changamoto zinakuja kipekee. Huo ndo ukubwa, na ukiwa mkubwa ni lazima uwe na ngozi ngumu. Maana yake ngozi ngumu inavumilia na kuhimili changamoto za kila siku unazokumbana nazo katika maisha yako iwe ya kikazi, mapenzi, elimu na mahusiano au taja chochote maana unaruhusiwa kutafasiri unavyoweza.

Usije ukaona simba kanyeshewa ukadhani paka na ukataka kumkumbatia kumfuta maji, simba ni simba atakurarua hapendi kukumbatiwa, muache afanye yake kama haingilii njia zako za maisha na ikitokea akaingilia niia zako basi usisiste kumtoa njiani na kumpeleka panapomfaa. Tafasiri unavyoweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…