Makapuku Forum

Muziki: Baada ya Pasaka na Winnie

Mapumziko ya Pasaka yamekwisha na leo kwa wengi ilikuwa ndo siku ya kwanza ya kazi katika wiki. Siku nne za mapumziko si haba, yaani kama umetemebelewa na mgeni unaanza kuwaza ataondoka lini. Nikusalimie kapuku mheshimika na kukutakia pole kwa mihangaiko ya leo, najiaminisha kabisa kama kuna siku umechacharika kiukweli basi ni leo maana sikukuu imekuachania mifuko na bahati mbaya sana ATCL hawakutoa ndege za kwenda kuhudhuria mapokezi ya ndege yetu.

Pasaka hii imeambatana na msiba mzito kwa taifa la SA na Afrika nzima kwa ujumla. Msiba wa Winnie M. Mandela, mwanamama wa nguvu, mpigania haki za watu weusi huko bondeni. Kifo chake kimeacha majonzi lakini matendo yake na kujitoa kwake kama mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi utabaki kuwa ni alama kuu ya vzazi vijavyo ukiachana na makndokando mengine ya kibinadamu. Pumzika Winne

Muziki sasa. Nikutakie wakati mzuri

 
Shikamoo binamu[emoji134] [emoji134] [emoji134]
 
Mtaasisi mwenzangu Nyagei heshima nyingi sana kwako na kile kibao cha Yori yori sio kwamba nilikisahau sema tu kuna masuala ya kiufundi na mtando yaliingiliana nikashindwa kupandisha muziki hata hivyo nilijua kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha kuelekea pasaka basi uliburudika na mengi ukiacha muziki.

Pamoja sana
 
Muziki: Karanga Zenye Michanga

Wiki inakwenda kasi sana, huwezi kuamini majuzi kuna wadau walikuwa wamefunga na sasa wamerudia maisha yao ya kawaida, yale maisha waliyoyazoea na kuwafanya wawe wao kama wao na si kuiga majina ya kwenye vitabu. Ninakusalimia Kapuku mwenzangu na kukuambia tu kuwa japo hujauliza siku yangu ilikuwa nzuri sana, asante kwa kutouliza. Ninajiaminisha ulikuwa na siku nzuri pia, karibu hata kama hujaniambia asante. Siwezi kuacha kukushukuru wewe kwa kuwepo hapa, unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri sana kuwepo.

Nilikuwa naongea na anko wangu Lyon Lee ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni, hivi kuna wau wa ajabau kweli, yaani mtu anachukua likizo kipindi cha Aprili, kweli!!! Lakini nisiseme sana lakini ndo anko wangu kachukua likizo, ila kasema hataki kusafiri maana akisafiri tu mipango yake inachelewa. Hapa somo ni kuwa likizo japo inapendeza kusafiri hakuna ubaya usiposafiri, simu si zipo bhana.

Muziki sasa, nakusalimia Tumosa mama JJ na kukuambia unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Furahia muziki maana wote wanaosema kitumbua kikiingia mchanga hakiliki, hawajajaribu karanga

 
Baada ya United kushinda Kwa cleansheet Easter ikawa much blessed, honestly nilifurahia mapumziko japo nilimiss muziki mzuri toka kwako Dj mtaasisi
 
Anfield ni kwa mwanaume kamili kumpiga City 3-0 sio jambo dogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…