Makapuku Forum

[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji7]
 
Tafasiri Unavyoweza: Taswira Darajani

Kila mmoja wetu ana historia ambayo inapendeza wengine wakaijuana hasa watoto. Kwanini nasema hivi, najiaminisha kuwa wengi wetu humu tuna umri wa kitaifa na wengine tumeanza kukaribia kutoka kwenye umri wa kijana. Katika hatua zote hizi tumepitia mengi na tuna mengi ya kushirikisha wengine na hasa watoto wayafahamu, itawasaidia sana katika makuzi yao. Itawafanya wawe na maisha yanayofaa kwenye jamii. Kumbuka akili ya mtoto hukuzwa na wanaomzunguka na uwepo wako humu Jukwaani inaonesha kuwa wewe ni mtu makini, vinginevyo hata usingikuwa na ruhusa ya kuandika na kusoma unayopenda hapa. Tafasiri unavyoweza.

Taswira darajani inaega kukuonesha kuwa ni namna gani wewe unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko kwa mtoto, ndiyo, pale utakapochukua kalamu na karatasi na kuamua kuandika kitu, iwe shairi, ngonjera, nyimbo au hadithi. Naandika haya nikijua kabisa kuandika si jambo rahisi na hasa kuandika tunzi zisomwe na watoto (crafting a children book is not easy, need creative skills into creating a successful story). Lakini, kwa maisha ambayo umeyapitia huwezi kushindwa kuandika kitu ambacho kitamsaidia mtoto wa Taifa hili.

Sisi ni walezi wa watoto kwa nafasi za majina yetu tofauti iwe baba, mama, mjomba, shangazi na jina lolote lile linalokufanya uwajibike kwa mtoto wa Tanzania, andika kitu, mfanye mtoto asome na itamjengea uwezo wa kufikiri na kuwa mdadisi (inquisitive) na hili ni afya kwa jamii na taifa letu. Tafasiri unavyoweza
 
Muziki: Ukikunja Ngumi Hufikiri Sawasawa


...kufikiri ni mchakato/ process na si jambo linalohitaji nguvu ya mwili zaidi (physique-tamka fiz-eek) bali utambuzi, nguvu ya kuchambua mambo na zaidi nguvu ya akili timamu. Ninakusalimia Kapuku mwenzangu na kukwambia tu it is almost Furahiday.

Siku nyingi sijaandika mengi hapa, naweka muziki tu na kuacha muziki uongee, si unamkumbuka Hamza Kalala na kile kibwagizo chake cha eee mamama tunakula miziki' ndo nilikuwa nafanya. Na huu ulikuwa ni ushauri wa anko wangu Lyon Lee ambaye kwa kweli amekuwa kwenye wakati mgumu sana kipindi hiki maana ukiacha safari zake za kanda ya kaskazini bado hata huku JF alikuwa akipambana na waandamanaji waliojipanga kimkakati kukaa wanamsifia aunt yangu.

Muziki, niseme tu Makapuku forum ni sehemu nzuri kuwepo na ukisoma kipenegele hiki utajijua wewe ni mtu muhimu namna gani humu Jukwaani.

 
Ahsante sana mtaasisi kwa kibao cha Loi toka kwa mkali wa zamani Olomide
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…