Tafasiri Unavyoweza: Siku ya Wanawake Wanatangulia Wanaume, Safari Bado Ndefu
Kila jinsi (sex) na siku yake, ipo siku ya wanaume na leo ni siku ya wanawake, wapo kwenye siku yao na siku hii ina historia ya kuvutia kusoma. Ilianza kuadhimishwa nchi za Magharibi na kusambaa zaidi karne ya 20, kuanzia magharibi hakumaanishi Africa, Tanzania kwa mfano na makabila yake hayakuwa yakithamini wanawake na kuwakumbuka kila mwaka kwa sherehe na mambo mengi mengine. Fuatilia jinsi makabila yetu yanavyomchukulia mwanamke na hapa ndipo utajua kuna jambo zuri kujifunza wengine wanafanya nini kuwaenzi wanawake zao na sisi tunafanya nini kuwaenzi wanawake katika jamii etu. Binafsi natoka kwenye kabila ambalo mwanamke ana nafasi kubwa ya kuitengeneza asubuhi yako na kukuletea jioni nzuri ukimheshimu na hata kusalimiana tunasalimiana kwa jina la mwanamke. Tafasiri unavyoweza.
Bado kuna changamoto kubwa sana ya usawa wa kijinsia katika jamii yetu leo, wanawake walio wengi wanaishi kwenye umaskini na utegemezi usio na mfano ukilinganisha na wanaume. Ndiyo, wapo wanawake wenye madaraka makubwa nchini na wengine wanashika nafasi nyeti za maamuzi katika jamii lakini unajua takwimu za sensa zinaonesha kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume na vipi sasa uwiano kwenye vyombo vikubwa vya maamuzi kama bunge, serikali na mahakama idadi yao ni ndogo sana, tafasiri unavyoweza. Kuna vikwazo vingi wanakumbana navyo kuanzia ndani ya nyumba, kwenye nyumba za ibada, shuleni, makazini na hata serikalini. Tafadhari bila kulali wewe ni mwanamke au mwanaume usiwe kikwazo cha kuifikia safari ya usawa wa kijinsia
Sijamaliza kuandika nikiamini kabisa utamalizia maana nimeandika kama kuchokoza tu mada na kukufanya utafasiri unavyoweza katika kusheherekea siku hii nzuri ya wanawake kimataifa. Ukijitafakarisha ni vipi pamoja na kelele nyingi za usawa wa kijinsia bado kundi kubwa la watu kiidadi linaongoza kwa umaskini, kukosa elimu, utegemezi, kuonewa kisheria na zaidi kunyanyaswa kijinsia. Tafakari na tafasiri unavyoweza.
Hongera wanawake wote mlio Makapuku forum,
BlessedHope ,
Jimena ,
Shunie ,
husna muba ,
ABJ ,
demi Valentina ,
Sakayo ,
Clkey ,
Tumosa ,
Linamo ,
Madame S , na wewe mwanamke ambaye sijakutaja jina lako ila amini tu kuwa wewe unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri sana kuwepo. Hongera na endelea kufurahia siku hii