yaani nimependa mpaka naumwa yani, na kitu ambacho sikukitarajia kabisa yani"
"mapenzi ni upofu mama... Ndo ushapenda hivyo"
Lakini sasa Rose akiwa anaongea hivyo huku alikuwa kama anabinua mdomo kana kwamba hajapenda ishu kama hio... Kuna kijiba roho kinaanza kati yao, na yote hayo kisa ni mwanaume tu... Ngoja tuone mwisho wao..
Tukija huku kwa mama zaituni akiwa na sheby pembezoni mwa ukuta wa nyumba yao, wakati huo inakwenda mida ya saa nne hivi usiku, kijana sheby anazidi kuchelewa kwao bila kujua kule nyumbani wazazi wake tayari wamesha chafukwa juu yake,..
"baba... Mimi nimekubali, lakini sasa utaishi ishi vipi nae"
Aliongea mama zai huku sheby akicheka sana,
"kikubwa ni ruksa yako tu.. Na tutafanya mipango ya ndoa kabisa lakini sio sasa hivi"
"kweli una nia njema na mtoto wangu... Lakini sasa kabla ya hio ndoa yenu mtoto wangu ataishi wapi.. Mana akiendelea kuishi hapa kwangu atakufa"
Mama aliongea jambo lililomshtua sheby...
"Ati nini... Afe???... Auwawe na nani"
"sio Auwawe na nani... Ivi kumbe hajakwambia"
"aaakuuu mimi sijui... Kwani kuna nini"
Sheby alikuwa tayari kuskia sababu ya kifo kwa zaituni pindi atakapoishi hapo
"ivi unajua kiwa huyu zaituni kamwagiwa tindikali na dada yake ambae ni pacha wake"
"Whaaaat"
Sasa Sheby yeye alikuwa hajui hii ishu kama upofu wa zaituni ulisababishwa na zainabu.. Sasa leo ndio anatobolewa siri
"ndio.. Na sababu ya kumwagia ndugu yake, ni hii hii ya mambo ya wachumba... Nakumbuka kuna kioindi nilikuwa sijiwezi, hivyo nikawaambia kila mmoja sasa atafute mchumba aolewe, lakini sasa zaituni ndio aliokuwa anapata posa nyingi kuliko zainabu,.. Na zaituni yeye hakiwa akitaka kuolewa hivyo posa zote akawa anazikataa eti mpaka afikie malengo yake... Lakini sasa kumbe dada yake zainabu anaona wivu na jambo lile, hivyo alifikia hatua ya kumwagia ndugu yake tindikali ili zile posa zimjie yeye.. Sasa na wewe ukiweka nia kama hio atauwawa kabisa, mana alifanya hivyo ili asiolewe, sasa kama wewe umejitokeza baba... Afu unasema tutafanya mipango ya ndoa baadaye huoni atamuua kabisa"
"mungu wangu weeeeee....ivi una uhakika na yeye ni mtoto wako kweli"
"baba, nimewazaa mwenyewe tumbo moja na walikuwa pamoja"
"sasa si umfukuze... Kwanini ukae na mtu kama huyo.. Mtu katili kiasi hicho unaishi nae vipi sasa"
Sheby alikasirika sana kuskia kuwa yule aliotaka kumbandua kwenye gari ndio aliosababisha upofu kwa ndugu yake,..
"kumfukuza siwezi.. Kwasababu kuna vitu anafanya na bila yeye hatujui tutaishi vipi"
"kwahio upo tayari familia iishe kwasababu ya hicho kitu mama... Kwani ni kitu gani hicho"
"mmmhhhh baba,.. Tuyaache tu hayo"
"we niambie mama angu, huenda nikaweza kukuseidia japo kidogo tu"
Sheby alijikuta anaingilia majukumu mengine ambayo hayakuwa yakimuhusu kwa yeyote ile,... Mama anasita kuongea, kana kwamba jambo analofanya zainabu ni kubwa sana na hata sheby hatoliweza kulifanya...
"baba, nakuonea huruma sana... Sidhani kama utaweza baba"
Hata sheby mwenyewe alianza kuogopa kuhusiana na jambo hilo, alijikuta anarudi nyuma, kwani hata huyo mama alianza kumwogopa, mana ni jambo gani analoweza kufanya mwanamke afu mwanaume ashindwe???... Sheby aliogopa na kutia hofu kubwa sana ndani ya moyo wake.. Alihisi kuna jambo kubwa hapa...
"basi mama usiseme tena.. Tuyaache hayo mambo"
Lakini sasa kabla sheby hajataka kuondoka,... Ghafla zaituni alitokea na kusema kuwa
"mama kama hutaki kumwambia ukweli bora mimi nimwambie kuliko kuishi na jambazi humu ndani"
Itaendeleaa....