Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Darasa La Saba

Leo ni siku nzuri sana, yeah, ni furahiday, watu tulienda kupiga mkeka, eeeh ukisikia mkeka vijana wa humu mnajua ni mambo ya betting, mimi huwa sibet, hata mjomba wangu huwa habet, hafanyi huo upuuzi labda abet kwenye masuala ya kimwili. Kwanini namsema anko wangu habet, majuzi kasema habeti kumbe habeti kwenye mpira ila kimwili akamtumia mhamiaji haramu mmoja nauli toka namanga kuja alipo (sipataji alipo mjomba wangu kwa sasa hadi hapo baadaye), si ndo kubet kwenyewe huko.

Basi bhana, matokeo ya LY yaani std 7 mika yangu ilikuwa ni siku ya balaa kwa sababu my friend kachaguliwa kusoma shule ya serikali wakati mimi hata jina langu halikuonekana mwanzo wa majina hadi mwisho. Nikajiuliza je hawakusahihisha paper zangu au vipi nimefanyiwa hiyana maana kwa kutoroka kwenda kuiba mahindi na kucheza mpira nilikuwa bingwa. Nadhani kama umitashumita ungekuwa unafanyiwa mtihani wa mahudhurio ningekuwa Tanzania One ila ndo hivyo nilifanyiwa mtimanyongo paper langu halikuonekana maana yametokeza majina 100,000+ langu halimo, wasio wazalendo wakasema sikufaulu. Nikarudi kuendelea na mambo ya mipira. Na leo nipo hapa nimekuwa kocha wa veterani

Muziki sasa, leo nimeandika sana maana ni ijumaa ya matokeo ya std seven, nimekumbuka mengi maana walimu baada ya kunisisitiza niwe nakaa mbele ili niwe na akili wakaniacha nikawa back bencher.

Binamu asante sana muhenga me umenikumbusha mbali enzi za nyimbo hii ilivyokuwa inatamba halaf binamu naomba kesho tukutane central
 
...utakauka mate bure, kuku ni kweli aliahidiwa lakini akatokea penzi jipya akapewa. Mimi nilijitahidi kumsisitiza anko atimize ahadi, akatishia kunisomea albadiri nikaona isiwe tabu, nikambeba kuku na nikamchinjia kabisa penzi jipya.

Labda nimletee manyoya ili angalau apate cha kujichokonolea sikio
Binamu una nini jaman na huyu kuku ninaeletewa ni vipiii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom