Makapuku Forum

Makapuku Forum

3ca28b1c16d188bd56977033a69a369c.jpg
 
Muziki wa Wikend: Kama Jana Unaiita Zamani, Kesho Utaiitaje?

........nakusalimia ama baada ya salamu mimi ni mzima wa siha njema. Hofu kwako wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu. Ninakukumbuka sana Kapuku mwenzangu yaani hadi mtima wangu unalia ndu ndu ndu, na usichanganye mdundo huu na lile daraja la Ndundu.

Unataka niseme nini kwako wewe uliyelifanya Jukwaa likawa juu kama mkata umeme wa Tanesco? Kapuku Forum ni sehemu nzuri kwa sababu wewe upo na unalijua hilo, asante kwa magazeti, sala, UF, BBC, historia, sports na sogozi ambazo zimetufanya tuwe na wakati mzuri.

Wikend hatuna mengi sana na jitahidi unitumie simu ya barua maana ukinijibu kwa posta itachukua muda, barua zangu zinapitia sanduku la shule na unakumbuka mambo ya c/oSM Shamaliwa, Nyakato Mza. Na ukinidipu stojua umenipigia maana posta na simu bado zimeungana.

Tuburudike na muziki wa zamani japo meseji hazijabadilika yaani kama EMS, TMO, Fax na kulamba stamp.




Na usisahau vijimambo vya mtaani baada ya kumaliza shule


Ahsante mdau


Ungejua upuuzi walioufanya TANESCO leo bora usingewataja kabisa
....
....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom