Makapuku Forum

Gospel Time: Jumapili Tulivu

Ninakusalimia Kapuku mheshimika, najua una wakati mzuri Jumapili hii. Asante kwa Higher Power kutupa nafasi ya sisi kuwa hapa. Nitarudia tena gospel music huwa haijali dini hata kama ziko zinahusiana na ukristo zaidi. Ni muziki mzuri kuusikiliza na unaburudisha na ndiyo maana hata kwenye Jukebox tunazichaguaga huku tunaangusha moja moja na tukifurahia tunasimama tunacheza kwa step.

Anaitwa Shusho, anajulikana sana kwa nyimbo zake nzuri zinazovutia. Sauti yake inaendana na sura yake na umbo lake la umiss bantu basi mimi naandika hapa huku natamani ningekuwa namtungia mashairi. Mungu azidi kumbariki sana. Usinihukumu kabla hujahukumiwa, burudika

 
Asante binamu yangu
ubarikiwe sana sana si unajua vene nakupenda
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…