Makapuku Forum

DHK. ...
KWA WALE WAPENZI WA KAHAWA


.......Unywaji wa kahawa hurefusha maisha
Ni habari njema kwa watumiaji wa kahawa, kwani utafiti uliofanywa hivi karibuni , umebainisha kwamba watu hao wana uwezekano wa kuishi maisha marefu zaidi.

Utafiti huo unaeleza kwamba watu wanaokunywa kati ya vikombe viwili na vitatu, hupunguza hatari ya kifo kwa asilimi 18 wakilinganishwa na wale wasiofanya hivyo.

Kiongozi wa utafiti huo, Profesa Veronica Wendy Setiawan wa Chuo Kikuu cha Southern Califonia (USC), alisema licha ya tofauti ya mfumo wa maisha, hali iko hivyo kwa makundi yote.

Matokeo hayo yanaonyesha uwapo wa uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya kinywaji hicho na maisha marefu kutokana na kupunguza uwezekano wa maambukizi ya maradhi ya moyo, saratani, mfumo wa kupumua, kisukari, kiharusi na figo.

Utafiti huo uliwashirikisha zaidi ya watu 185,000 wa asili tofauti kwenye majimbo mbalimbali nchini Marekani na matokeo yakawa sawa.(CNN)
 

Ni mtandao usio wa wauza sura hivyo waswahili huupotezea na kuzamia Facebook na Install
Nasikia bongo Reginald Mengi anaongoza kwa followers ila JK naye yumo
......
Kwa utafiti wangu usio rasmi nimegundua wabongo wengi wapenda maneno mengi swaga nyingi kule hakuna maana maneno kwenye posti nzima ni 140.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…