Tottenham wamesema hawatoburuzwa na Manchester United na Manchester City kuhusu usajili wa Eric Dier na Kyle Walker, huku wakikaribia kumsajili beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 9. (Daily Telegraph)
Manchester United sasa wataelekeza nguvu zao kumsajili kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 29, kwa kutoa pauni milioni 40 baada ya Tottenham kukataa dau lolote kuhusu Eric Dier. (Daily Mail)
Leicester City huenda wakaondoa wachezaji sita waliosajiliwa msimu uliopita akiwemo Islam Slimani, 29, na Ahmed Musa, 24, pamoja na kiungo Nampalys Mendy, 25. (Daily Telegraph)
West Ham wanafikiria kupanda dau la tatu kumtaka Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la pauni milioni 20 kukataliwa na Stoke City. (London Evening Standard)
Manchester City wanataka kupanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki wa Southampton Ryan Bertrand, 27, baada ya kumkosa Dani Alves aliyesaini PSG. (Daily Mail)