Chelsea wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kwa pauni milioni 60 baada ya Tianjin Quanjian ya China kusema haitaki tena kumsajili mchezaji huyo. (Daily Mail)
Borussia Dortmund huenda wakaamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, ambaye pia anasakwa na Everton, West Ham, Marseille na AC Milan. (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, amempigia simu meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuambia hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu huu. (Diario Gol)
Meneja wa Chelsea anajiandaa kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwa pauni milioni 40. Matic amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford. (Daily Telegraph)