Muziki: Jipange
Ni siku nyingie tena baada ya mapumziko ya Eid! Natumaini sote tulikuwa na wakati mzuri wakati wa mapumziko ya sikukuu hii maarufu. Wale tuliokula kukapitiliza, safi mmeweka kumbukumbu, wale tuliokunywa, hongera kwetu na hongera zaidi kwa wote mlionunua na kuvaa nguo mpya wakati wa sikukuu. Yeah, nani hapendi kula na kunywa, kuvaa na kupendeza, nani?
Jukwani hapa tulipotea, mliokuwepo mtakumbuka visingizio kibao, ooh mara ooh, mbuzi zangu zinataka chapati sikukuu hii, oh mara historia hakuna siku hii ilmradi tu kila sababu ilitafutwa kuhalalisha mapumziko ya sikukuu. Sikumbuki nilitoa sababu gani nikaakcha kuweka muziki, ila naamini ilitosha kabisa kupata mwaliko wa Eid.
Ni jambo zuri humu KF kuwaona wadau wakiwa wamerejea tena,
Nyagei ,
mzeewakungoa ,
Transcend ,
werrason na wote, karibuni sana. Its great to have you here good pipo. Asante
Jimena kwa kumbukumbu ya ilipotokea KF, binafsi sikumbuki niliingiajeingiaje huku, lakini ni sehemu nzuri kuwa kwa kuwa tu wewe mpenzi msomaji na Kapuku mwenzangu u sehemu yake.
Muziki sasa, huwa nikimuona huyu dada akipiga gitaa nakumbuka miaka ile Grace Matata (free soul) akiimba, anakatiza pale mitaa ya kwa Urassa (ni kigamboni) akiwa na gitaa lake na virasta vyake vifupi vikipeperushwa na upepo wa kigamboni. Oh yes, kigamboni tunasubiri panton, tukishangaa meli.
Ila simuongelei huyu Grace leo, namwongelea mdada maarufu kabisa huko SA kwa ASS (After Sex Shower) , usigune ni Zuma huyo alisema ukimaliza oga hutopata ukimwi, really!
Mdada mpiga gitaa na mwenye sauti inayoendana na nyuzi za gitaa anaitwa Zahara, ninaweza kumwandika sana lakini haitoshi kusema baada ya Brenda Fassie kuuza nakala nyingi, alifuatiwa kwa ukaribu zaidi na mwanadada Zahara. napenda kibao chake kinaitwa Nd'iza.
Ila mwangalie hapa leo katika Loliwe (uzuri kizuri kinaubantu mwingi unaweza kukutana na kilugha chenu)