Makapuku Forum

Makapuku. Itabidi tu niwaombe radhi. Topiki ya Falsafa sitaweza kuianzisha leo. I chewed more than I can swallow. Kumbe inabidi nisome some kidogo vinginevyo nitaishia kuwaletea mawazo yaliyofinyangwa finyangwa tu kiholela. Na mimi huwa sipendi mediocrity.

Lengo langu la ndani katika topiki hii ni mimi kujifunza zaidi kuhusu falsafa kwa sababu itabidi nijisomee kwanza. Ni katika jitihada za kupanua mawazo tu kwani huwa navutiwa sana na wanafalsafa mbalimbali hasa Emmanuel Kant (mwanzilishi wa tapo la Existentialism), mwanafalsafa kichaa Fredrick Nietzsche (huyu aliwahi kuutangazia ulimwengu kuwa God is dead!) na wengineo wengi.

Kwa hiyo Falsafa itaanza wikendi ijayo Jumamosi na nitaanza na mawazo juu ya kifo na jinsi kinavyotazamwa kifalsafa. Je, wanafalsafa wanakionaje? Tunapaswa kukiogopa kifo? Tufanye nini? Asanteni....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…