Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki Mpya wa Zamani.

Ni Jumamosi leo, kwa wale wote msiokuwa na uwezo wa kumiliki kalenda, na kiukweli leo nilitamani sana nimwage yai (niandike/kuongea kiinglishi) lakini kila nikifungua mdomo, ulimi unagoma kabisa. Inawezekana kinywaji nilichokunywa a day before yaani yesterday mchanganya kilevi alikuwa ni mswahiliswahili hivi. Hongera sana ambao mkilewa ndo kingereza kinapanda.

Nimekaa napumzika hapa nikawa najiuliza muda huu Makapuku tumezoeshwa kupata oldies toka kwa Sweetiepie ambaye ana ahadi kama mbunge wangu tu. Anyway , who knows she might come back with a bang. Usicheke, nilikaa mahali ikanilazimu kuongea kiinglish wiki nzima, nilikonda sana.

Mapumziko ya leo ninakuletea muziki wa zamani ambao bila kusema uongo bado unabamba sana hadi leo, kitafute kibao cha Mapenzi Yananivunja Mgongo then utaniambia kama hukutekenyeshwa masikio. Hata hivyo kwa kuwa nia na sababu ya kushindwa kuongea/kuandika kiinglishi haijanifanya nishindwe kusikia maneno ya muziki unaoimbwa 'kizungu'.

When a Man Loves a Woman' ni kibao kilichompatia sifa sana MB na kiasi cha kudhani kuwa mtunzo ni Michael Bolton (nilishamweka humu). basi katika pekua pekua nikakutana na gwiji mtaalam Percy Sledge, oh yeah yeye ndo mtunzi wa hicho kibao na alikirekodi mwaka 1966, enzi hizo hakuna cha MB wala GB ni mwendo wa taipuleta tu.

Kibao hiki alikiandika makusudically kabisa kuonesha machungu dhaidi ya hatua ya mpenzi wake ambaye alimwacha (kumpiga kibuti) baaday ya yeye, Percy kupunguzwa kazi aliyokuwa akifanya. Unafukuzwa kazi na kisha unaachwa na mpenzi wako, yaani ni kama timu za Yanga na Simba na pesa za SpotiPesa..

Nakuwekea clip hii ya YouTube ambapo Percy kaimba na Michael

 
Weee cheka tu, nitaibuka na kitu cha hatari hadi BH akubali kuwa mke wa tatu, yaani aje ananililia, usicheze na mpango ninaoukamilisha soon.

Ila BH akinikubali tu, kwanza kabisa naokoka, halafu ninakuwa naye peke yake
Tatizo lako binamu hujazingatia ushauri wa kukariri vifungu vya biblia,we nenda tu love connect huwenda ukabahatika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom