Sikonge amka kumekucha sasa,
Fanya uchunguzi utagundua kwamba Dunia nzima inaendeshwa kwa mfumo Katoliki wala si Kristo is just Catholic. Rudi uliza wana sheria watakueleza vyema uwezo wa Canon Law ulivyopenya kote.
Halafu MoU ile is jusy PPP amka cha kulialia wewe
Thubutu waondoe MOU uone kama zitajiendesha wanashindwa hata kufanya baadhi ya surgery sometimes kwasababu tu serikali haijapeleka fungu la MOU kwa ajili ya malipo ya wafanyakazi na ununuaji wa gas.Kama wangekuwa hawafaidiki wala wasingesaini MOU.Kwani kwenye hizo huduma za jamii pamoja na serikali kuwekeza ni wapi umeambiwa makanisa wanatoa huduma hizo bure au kwa bei nafuu?Kutokana na kulalamikiwa saana na Waislaam kuwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa (MOU) yanafanya nchi hii iwe na "Mfumo Kristo" na hivyo kuwanyanyasa Waislaam na hata kuwatawala, inabidi ifike wakati Makanisa yaanze kufikiria jinsi ya kuvunja mkataba huo na kurudi kama ilivyokuwa zamani.
Kwa sababu hili swala limeonakana likichochea sana vurugu, mie napendekeza lifuatalo:
- Wavunje mkataba wa MOU na Serikali.
-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mahospital ya Kanisa.
-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.
-Makanisa na vitengo vyake, viwe vinalipa kodi kwa kufanya biashara ya Hospitals, Shule nk.
-Gharama kwa walio Wakristo, ziwe zinapunguzwa kwa wingi kwa sababu wao hutoa michango mingi tu ya kuendeleza kanisa na sadaka za kila Jumapili.
-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.
Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.
Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.
Kama kuna kundi jingine au Serikali litakuja na mbinu mbadala na kuweka huduma hizi za jamii katika bei nafuu zaidi, basi ina maana huduma za jamii kutoka kwenye Makanisa tutakuwa hatuhitaji tena. Maendeleo yanakuja kwa mashindano. Muda umefika Makanisa kutangaza mashindano kwa kutoa huduma za JAMII VS dini nyingine au Serikali.
--
Hizo hospitali kubwa zote unazozitaja serikali ndiyo iliyozifikisha hapo zilipo na Mh. Rais Mstaafu Mkapa kutaka kuficha mabaya yake akaamua kuyapatia makanisa na awali zilitaifishwa na Mwalimu na zilipotaifishwa na kuchukuliwa na serikali zilikuwa ktk hali duni serikali ikafanya mabweresho na Mkapa akazirudisha kinyemela kutaka kuficha zile biashara alizokuwa anazifanya ikulu na kawaziba mdomo kina Kitwana Kondo akatoa majengo ya Tanesco kuwapa the so called muslim university!Nadhani amelala huyo! Hajui kwamba KCMC, Bugando ambazo ni hosp kubwa nchini zinatoa msaada tu! Mbona viwanja vipo kwanini sisi Waislam tusifunguke? Tuna Morogoro University, hivi tumefanya nini cha maana tangu Mzee wetu Mkapa atupatie yale majengo bure? HAdi leo hatjawahi kuyakarabati!
أنها وفرت لنا، ونحن نقدم ثيقة من وثائق اتحاد تنجانيقا وزنجبار
Kanisa limewahi kuendesha mashule na mahospitali yake bila ya MOU ni busara sasa kanisa na hata taasisi za Aghakan foundation zijitoe kwenye mkataba huo kisha kanisa lifanye biashara ya shule na hosptali ambapo wale waliojenga mashule hayo na mahosptali wanaweza kupewa unafuu wa karo za shule na nafuu ya kulipia tiba.
Hofu yangu ni kwamba kwa kuwa nchi imeanza kuvurugika kidini kuna ishara kwamba baada MOU kuvunjika kanisa linaweza kutoa vitambulisho kwa waumini wake ili wasome kwa nafuu na kutibiwa kwa nafuu na wasio waumini wa kanisa watalipa gharama za juu.
Hii inawezekana kutokana na imani kwamba wakati huo fedha za sadaka, zaka, harambee, mavuno na minada ya kanisani itakuwa inaendesha huduma hizo na serikali haitakuwa na mkono wake katika huduma za kidini.
nani kasema nhif ni hosptl?
Nimesema watibiwe kwenye hosptl yoyote iwe binafsi au ya kanisa kwa kutumia bima kakini baada ya serekali kuvunja mou na kanisa.
Mkuu Sikonge, ni kama vile ulikuwa kwenye mawazo yangu. Lakini je na makanisa hayo yatazizuia taasisi zake kutoa huduma za afya na elimu kwa watu wasiokuwa wa madhehebu yao?
Ni ukweli kabisa hilo litaondoa mzizi wa fitina, ila pia kutakuwepo na madhara yake mengi tu. Especially kama kuna watu wasiokuwa wa madhehebu hayo ambao bado walikuwa wakipata unafuu wa huduma hizo kutokana na msaada mmoja wa serikali kwenye uchangiaji wa kuendesha huduma hizo.
Hatahivyo bottomline nakubaliana na wewe.
[h=2]Ridhiwan Kikwete na "utajiri wa kutupwa"[/h]https://www.jamiiforums.com/habari-...4-ridhiwan-kikwete-na-utajiri-wa-kutupwa.html
Sawa kabisa Mkuu. Ridhiwan hela zake zote zinaishia Kanisani. Ramadhani Dau ndiyo nasikia hata Account zake zite kawakabidhi viongozi wa kanisa, Halleluyah......