Temporary01
JF-Expert Member
- May 12, 2011
- 260
- 70
Serikali haijashindwa, tatizo ni kwamba haijaamua.Serikali imeshindwa kujenga hospitali na shule kukidhi mahitaji ya nchi ndio maana kuna ongezeko kubwa sana la hospitali na shule binafsi. Rejea hotuba ya JK kwa Wauslamu huko Dodoma.
hilo la gharama kubwa mbona lipo siku zote,upo nchi gani?makanisa mmezidi na hamjui kula na kipofu.Mbona hiyo sasa itakuwa ni biashara nzuri sana kwa kanisa? Maana bila pesa hakuna matibabu. Watajipangia gharama kubwa wanayotaka. Aliye maskini shauri yake!!!
Bora tusiyachoma makanisa, kwa sababu kodi itaongezeka na ufisadi utaongezeka ili wakuu wakina Edward na wakiristo wengine wezi wakachangie makanisani
Kutokana na kulalamikiwa saana na Waislaam kuwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa (MOU) yanafanya nchi hii iwe na "Mfumo Kristo" na hivyo kuwanyanyasa Waislaam na hata kuwatawala, inabidi ifike wakati Makanisa yaanze kufikiria jinsi ya kuvunja mkataba huo na kurudi kama ilivyokuwa zamani.
Kwa sababu hili swala limeonakana likichochea sana vurugu, mie napendekeza lifuatalo:
- Wavunje mkataba wa MOU na Serikali.
-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mahospital ya Kanisa.
-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.
-Makanisa na vitengo vyake, viwe vinalipa kodi kwa kufanya biashara ya Hospitals, Shule nk.
-Gharama kwa walio Wakristo, ziwe zinapunguzwa kwa wingi kwa sababu wao hutoa michango mingi tu ya kuendeleza kanisa na sadaka za kila Jumapili.
-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.
Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.
Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.
Kama kuna kundi jingine au Serikali litakuja na mbinu mbadala na kuweka huduma hizi za jamii katika bei nafuu zaidi, basi ina maana huduma za jamii kutoka kwenye Makanisa tutakuwa hatuhitaji tena. Maendeleo yanakuja kwa mashindano. Muda umefika Makanisa kutangaza mashindano kwa kutoa huduma za JAMII VS dini nyingine au Serikali.
--
Tatizo ni ELIMU
mbona vyuo wanavyosoma hawazungumzii? Tuweke limitation shule, vyuo walipe kwa ada ya kibiashara na vya serikali uwe mfumo ulliopo ili tuone kama watasoma. Pumbafu kabisa hawa wapenda misaada. Bahati mbaya wanaohitaji huduma hizi hawasemi na wasiohitaji ndo wanapiga kelele.
Nimekopi hiki kipande tu ili wote mnaopiga blah blah kuhusu MOU bila kufaham imekusanya nn ndani yake mpate kufunguka - Waislam hawapigi kelele za bure tu..Si kweli kwamba Serikali haipangi maendeleo yake kwa kuzingatia dini kwa sababu Serikali haina dini. Ukweli ni kwamba Serikali inapanga maendeleo yake kwa kuzingatia sana dini lakini ni ya kikristo.
Mfano ni ule mkataba wa maelewano baina ya Serikali na Kanisa (MOU), ahadi ya Serikali ni "Kushirikiana na Makanisa kupanga sera na maendeleo ya sekta ya Elimu, Afya na huduma za Jamiii." Je hii si mipango ya maendeleo.
Mkataba huo (MOU) umetoa mamlaka ya kuundwa kwa tume ya kikristo ya huduma ya Jamii (CSSC) kwa lengo la kuunda sera zinazofanana kwa huduma za makanisa na afya na elimu wa makubaliano na Serikali ya Tanzania. Pia mkataba huo umelenga kuwa na utekelezaji sawa kwa Serikali na makanisa katika maendeleo ya jamii. Je, huu si mpango wa maendeleo baina ya Serikali na Wakristo.
Katika kifungu cha 11 cha mkataba huo kinasema:
"Serikali ni lazima itoe nafasi za ajira katika vyuo vyake vya Ualimu (TTC) kwa Wakufunzi wa kikristo kufundisha watu wataofuzu kama Walimu kwa ajili ya shule za Makanisa zilizoanzishwa."
Je, hii si mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dini?
Kutokana na makubaliano hayo baina ya Serikali na kanisa, imelazimika Serikali kuyapa makanisa mabilioni ya fedha za wa-Tanzania kila mwaka katika utekelezaji wa mkataba huu. Mfano mwaka 2008 Serikali iliyapa makanisa jumla shilingi bilioni 170 (Gazeti la Jambo Leo la Jumapili 20/03/2011) liliandika hivi:
"Mwaka 2009 Serikali iliyapa makanisa shilingi bilioni 45. Mwaka 2010 iliyapa shilingi bilioni 61.9."
Kwa maana hiyo Serikali kuanzia 2008 hadi 2011 imeyapa makanisa na taasisi zake shilingi billioni 331. Jee Waislam na taasisi zake wamepewa nini?
Pia iweleweke kwamba zaidi ya asilimia 54 ya bajeti ya Wizara ya Afya inakwenda kwenye vituo vya Afya, zahanati, mahospitali na taasisi nyingine za afya za kikristo. Je fedha hizi zinaweza kutoka bila ya Serikali kuwa na mipango ya maendeleo?
Tatizo ni kufunika nywele muda wote na kuvaa pekosi hakuna hewa hakuna akili kufanya kazi vyema.
Serikali haijashindwa, tatizo ni kwamba haijaamua.
Kama imeweza kujenga kilomita elfu 18 za lami kwa miaka 8 tu dhidi ya efu 11 tangu tupate uhuru iweje ishindwe kujenga hosptl na shule?
Msiitetee serekali kwavile mnanufaika na MoU. Mbona kwenye kuwaongeza mishahara madaktari na waalim nyie ndo mlikuwa mkiilaumu serekali kuwa haitaki kuwapa madokta na waalim stahiki yao wakati uwezo inayo?
Iweje kwenye hili muitete serikali kama sio kwa vile mnanufaika?
Unachekesha kweli. Bima ya afya sio hospitali bali ni njia ya kuwezesha wewe kulipiwa gharama za hospitali baada ya kuwa umelipa premium. Sasa kama hakuna hospitali za kutoa huduma, utatibiwaje hata ukiwa na Bima ya afya kutoka makampuni 10?jmushi1
Mkuu hizo NSSF, NHC na nyinginezo zenye MoU na serikali ni taasisi za umma na hakuna asiyelijua hilo. Ziko pale kwaajili ya watanzania na hazina uhusiano wowote na dini.
Suala la kujiuliza, siku zote malalamiko ya MoU ya kanisa na serekali yametolewa lakini sio kanisa wala serekali lililotoa ufafanuzi, wanategemea watanzania tuamini nini kama sio kusadiki yanayosemwa na tunao ipinga MoU?
Tukisema kuvunja MoU kutaleta shida kwa watanzania wa kipato cha chini hiyo sio kweli kwasababu watatibiwa kwa kutumia bima ya afya ya NHIF kwa watumishi au CHF kwa watu wengine.
Mbona ukiwa na kadi ya NHIF unaenda hospital yoyote ya private kama Agakhan na unatibiwa?