Mkuu Mkapa alitoa chuo cha Tanesco kama kiini macho pesa aliwapa makanisa kupitia pesa za Mou zinajenga yale kama 100
bila ya wasiwasi wowote na nyingine zikabaki.
Chama
Gongo la mboto DSM
Kwanza nashukuru kwa kufunguka kuwa upo USA na siyo Gongolamboto kama unavyotuandikia.
Kwa kuwa unaishi huko, yanayotokea huku SIKONGE kwa kweli huyafahamu na unafikiri ni kama USA. Ni sawa na yule binti wa mfalme aliyesema "Kama watu wana njaa, si wale keki?"
Nilimjibu Barubaru kuwa kwa Sikonge hospital, Serikali inabidi ipeleke Tsh.20 milioni kwa mwezi ambazo ni sawa na Euro 10,000 sawa na mshahara wa Gavana wa BoT. Ila kwa sasa Sikonge Hospital inapokea Tsh. 00,000 milioni kwa mwezi.
Chama,
I respect you. Lakini kusema kuwa pesa za MOU zinatumika kujenga shule 100 za makanisa ni uwongo mtupu. Kwa hakika sijui ni hospitali ngapi ambazo serikali imeahidi kuzipa fedha kupitia MOU ambazo zinapokea fedha hizo, Kama alivyosema Sikonge, hospitali ya Moravian mpaka sasa inapokea zero money licha ya MOU. Na mimi naweza kukuthibitisha kuwa hospitali ya Shirati, as of July this year, ilikuwa haijapokea hata senti tano za serikali ingawa ni serikali hiyo hiyo iliomba hospitali ifanywe hospitali ya rufaa ya mkoa. Kwa hiyo dhana kwamba serikali inatoa MOU kwa taasisi za makanisa na makanisa kuzitumia kupanua himaya zake ni uwongo mtupu.
Sikonge,
Labda utudadavulie hizo Tsh 20 Million zipelekwe hospital kwa kazi gani? Je kwa ajili ya Amin cost au Ops Cost?
-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kusomeshwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.
Usiende huko!
Mahospitali,Makanisa,Shule vilivyojengwa na Mkoloni kwa hela ya Watanganyika wa dini zote viliachiwa Wakristo waendelee kuvimiliki baada ya Uhuru, Nyerere aliona mbali kuwa baadaye watu watakuja kuhoji hili hivyo akaleta ubabaishaji wa kujifanya kuvitaifisha baadaye kumuachia mwingine avirudishe!
MoU, Necta, Muungano ni vitu ambavyo Wakristo hawatokubali kwa gharama yoyote ile viingiliwe kwa sababu ndiyo mihimili yenyewe ya Mfumo Kristo
Kulijuwa hili ninalolisema angalia mtaharuki uliowapata wachangiaji hapa kuhusu hoja ya Kanisa kuvunja MoU na Serikali
Isikushangaze! Wakati Muingereza akija Tanganyika tayari kulikuwa na treaty kati ya nchi za Ulaya kwa jina la Ukristo (rejea historia ya tishio la Ottoman sultan, Selim 1 dhidi ya ukristo)!Kuna maelezo mengine yatolewayo humu yakiachwa yabaki hivyo yalivyo yanapotosha ukweli uliopo. Wewe Bwana unayejiita Sideeq dhana yako kuwa Mahospitali, makanisa na shule zinazomilikiwa na Makanisa zilijengwa na Mkoloni kwa hela ya Watanganyika wote si ya kweli hata kidogo. Naomba nitoe maelezo ya Kanisa Katoliki. Makanisa, Hospitali, vituo vya afya, zahanati, shule za msingi na sekondari vilijengwa wakati wa Ukoloni wa Mwingereza katika Tanganyika. Katika kipindi hicho isingewezekana serikali ya kikoloni ya Waingereza ikawapa Wakatoloki fedha za kujenga majengo kwa ajili ya kutoa huduma nilizozitaja hapo juu. Ikumbukwe kuwa Waingereza (wakiwa na dhehebu lao la Anglikana) wasingetoa fedha kwa ajili ya washindani wa dhehebu lao.
Jasusi mkuu wangu hizi zahanati msifikie kuzipa jina la Hospital. Hiyo Hospital ya Moravian inalaza wagonjwa wangapi na inatoa huduma zipi hasa hasi mkaipa masifa kemkem.. Je ipo ktk ubia na orodha ya CSSC ama ndio wameomba nawasubiri kukubaliwa kuwa chama maana hutujui ni zipi zinazo qualify kupata fedha za maendeleo. Kwa hiyo unaweza tu kuongezea kwa nini hii Hospital yaMoravian hawapewi lakini sii kwamba fedha haitolewi. Billioni 90 kwa mwaka unaweza fanya mengi sana kwa asasi moja.Chama,
I respect you. Lakini kusema kuwa pesa za MOU zinatumika kujenga shule 100 za makanisa ni uwongo mtupu. Kwa hakika sijui ni hospitali ngapi ambazo serikali imeahidi kuzipa fedha kupitia MOU ambazo zinapokea fedha hizo, Kama alivyosema Sikonge, hospitali ya Moravian mpaka sasa inapokea zero money licha ya MOU. Na mimi naweza kukuthibitisha kuwa hospitali ya Shirati, as of July this year, ilikuwa haijapokea hata senti tano za serikali ingawa ni serikali hiyo hiyo iliomba hospitali ifanywe hospitali ya rufaa ya mkoa. Kwa hiyo dhana kwamba serikali inatoa MOU kwa taasisi za makanisa na makanisa kuzitumia kupanua himaya zake ni uwongo mtupu.
kuna kanisa linasomesha bure waislam..au kwa bei nafuu ??! :confused2: kanisa gani hilo...? au shule gani hiyo ya kanisa inasomesha waislam bure/ kwa bei ya kawaida ..? naomba mfano ...
Mkuu Sikonge
Kwa pole sana kwa kumpoteza mzee wako kazi ya Mungu wote tupo njia moja Mungu amlaze mahala pema.
Turudi kwenye Mada husika; sijakataa hata siku moja taasisi iwe ya kidini au za kibinafsi; zisijitoleee; tunachokataa ni wizi wa rasimali zetu kwa kutumia mgongo wa dini; nilisema awali waathirika wa hizi pesa si waislamu tu; wapo wakristo wa madhebu mengine; waandishi wa MoU walikuwa ni watendaji wa serikalini kutoka madhehebu ya kikatoliki na waanglikana; jiulize kwanini Moravian na wasabato hawapewi? Mkuu binafsi kesho ukiniambia kuna mchango unahitajika wa kusaidia kuendesha hospitali ya Sikonge nitajitolea ni utashi binafsi; hata US nachangia shule kikatoliki ingawaje mimi si mkatoliki ipo kwenye maeneo ninayoishi na kuna wakati pia najitolea kwenye vijishughuli vidogo vidogo; mkuu sijawahi kuunga mkono wizi wa Marememeta; unakumbuka mzee jaji Warioba alivyozungukwa na kusaini kitu ambacho hakukijua hadi leo hana jibu kuhusu Merememeta; ndio hivyo hivyo mzee Mwinyi alivyozungukwa mkuu huu ni wizi nadhani unatetea kitu ambacho hukijui kaa chini tafuta data za hii kitu kinachoitwa MoU; mwanzoni nilikubaliana nazo baada ya kupata datas zake niliacha kinywa wazi; hapa hapana udini tunapigania maslahi ya taifa; yakishaundwa haya matabaka; zitakuwa vurugu ambazo kuzizima hatutaweza.
Chama
Gongo la mboto DSM
Hivi niulize kitu.. Kwa nini ndugu zangu wakristu mnapenda sana kutunga Uongo? Hivi kweli ndio mnaita ujanja wa waloelimika au mnataka tu kubishana..Kuna maelezo mengine yatolewayo humu yakiachwa yabaki hivyo yalivyo yanapotosha ukweli uliopo. Wewe Bwana unayejiita Sideeq dhana yako kuwa Mahospitali, makanisa na shule zinazomilikiwa na Makanisa zilijengwa na Mkoloni kwa hela ya Watanganyika wote si ya kweli hata kidogo. Naomba nitoe maelezo ya Kanisa Katoliki. Makanisa, Hospitali, vituo vya afya, zahanati, shule za msingi na sekondari vilijengwa wakati wa Ukoloni wa Mwingereza katika Tanganyika. Katika kipindi hicho isingewezekana serikali ya kikoloni ya Waingereza ikawapa Wakatoloki fedha za kujenga majengo kwa ajili ya kutoa huduma nilizozitaja hapo juu. Ikumbukwe kuwa Waingereza (wakiwa na dhehebu lao la Anglikana) wasingetoa fedha kwa ajili ya washindani wa dhehebu lao. Kitu kingine ambacho Bwana Sideeq unapaswa kujua ni kuwa wakati Wamisionari wa Kikatoliki walipokuja hapa Tanganyika walikuja chini ya miavuli ya mashirika yao ambayo ingawa kwa sheria za kanisa yalikuwa chini ya Papa, lakini yalikuwa tofauti. Kuna sehemu walikwenda Holy Ghost, sehemu nyingine walikwenda Wabenediktini, sehemu nyingine Wamisionari wa Afrika (White Fathers), Wakonsolata, Wajesuiti na kadhalika. Wengine kati yao walikuwa ni Wamonaki.
Hawa wote walikuwa na karama na misisitizo tofauti katika huduma zao za kimwili na kiroho kutegemea na shirika lenyewe. Mashirika mama yao huko Ulaya yaliwategemeza kwa kila kitu wakiwa hapa. Kipato cha Watanganyika wakati huo kilikuwa cha chini sana.
Makanisa yao na shule zao yalijengwa kwa fedha kutoka makao makuu ya mashirika hayo. Fedha walizopewa na makao makuu ya mashirika yao zilitolewa na waumini wa Ulaya kwa lengo la kuinjilisha nchi ambazo zilikuwa bado gizani kiimani. Hiyo desturi ya kupewa fedha kutoka Ulaya na Marekani haikuishia wakati wa ukoloni bali imeendelea hadi sasa. Katika maeneo ambayo watu wake wana umaskini wa kipato bado Wamisionari wameendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule, makanisa na vituo vya afya.
Kadri ninavyofahamu mimi, hiyo MoU si kwamba inalazimishwa na Kanisa Katoliki. Kwa miaka mingi hata kabla ya utaratibu wa kuingia na makubaliano na serikali Kanisa Katoliki limekuwa likitoa huduma hizo kwa kutoza kiasi kidogo cha fedha. Lengo lilikuwa si kufanya biashara bali kurudisha gharama ili huduma iwe endelevu. Hata hivyo katika sera ya afya ya nchi hii kuna aina ya huduma za afya hutolewa na serikali bila malipo. Huduma hizo ni kama chanjo kwa watoto chini ya miaka 5, huduma kwa mama na mtoto, hiduma ya tiba kwa wazee, huduma za VVU/UKIMWI, na kadhalika. Katika maeneo ambayo hakuna hospitali au vituo vya afya vya serikali ambavyo vingetoa huduma hizo lakini kulikuwepo hospitali binafsi ( za makanisa na wengineo) serikali iliamua kushirikiana na asasi hizo binafsi ili kuisaidia serikali kutoa huduma hizo. Huwezi kuwa na ushirikiano bila kuwa na makubaliano yatakayoonyesha mipaka ya majukumu kwa kila mshirika. Huu ndiyo mwanzo wa MoU.
Inawezekana kufuta makubaliano haya ya MoU. Matokeo ni kwamba huduma zitakazotolewa na asasi hizi za Kikatoliki hazitakuwa bure tena. Watalazimika kutoza fedha kidogo ili huduma ziwe endelevu. Itabidi sasa watoto wadogo na akina mama walipie kama ambavyo tunafanya kila siku tunapokwenda hospitali za watu binafsi.
Kwa Falsafa yake Kanisa katoliki haliwezi kuwabagua watu kwa misingi yoyote ile. Wote watalipa kiasi kile kile. Athari itakayofuatia hatua hii, hasa kwa kipindi cha muda mfupi na wa kati, ni kwamba lile lengo la kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kwa kasi litapungua. Kwa maneno mengine kasi ya vita dhidi ya magonjwa yanayosumbua watu wengi hasa mahali ambapo serikali bado haijafikisha huduma hizo itapungua.
Ninafahamu zipo hospitali na shule zinazomilikiwa na asasi za Kiislamu. Hizi nazo zimeingia makubaliano na serikali pia. Kadri ya ufahamu wangu kwa shule za sekondari za Kanisa ni juhudi ya Shirika, Parokia au Jimbo husika wakishirikiana na wazazi wanaojenga na kuendesha shule hizo. Serikali kama ina mchango wowote katika shule hizo hiyo itakuwa ni kwa shule zote bila kujali anayezimiliki. Sidhani kuwa ni asasi za kikatoliki tu ambazo hupendelewa kupewa ruzuku kama ipo.
Utamaduni na desturi ya kutoa huduma za elimu na afya kwa wanadamu ni wa zamani sana katika Kanisa Katoliki. Kwa kweli ni sehemu ya wito wake wa kuinjilisha wanadamu. Hata makubaliano yakivunjwa bado wataendelea kutekeleza wajibu huo. Kwa maneno mengine wataendelea kutoa huduma hizo kwa upana na weledi zaidi. Mwaka 2000 nilitembelea jimbo la Bamenda katika nchi ya Cameroon na kufahamishwa kuwa shule bora kabisa katika nchi ile zilikuwa mbili moja ya wavulana na nyingine ya wasichana na zote zilimilikiwa na Kanisa Katoliki. Kama utagundua sasa hivi Majimbo mengi ya Kanisa Katoliki yameanzisha shule nyingi sana za sekondari na hasa za wasichana.
Kwa kumalizia, majadiliano makali kuhusu makubaliano kati ya serikali na Wakritu pengine yanakuzwa sana. Mimi ningefikiri Waziri wa Elimu na Waziri wa Afya (ambao kwa bahati nzuri ni Waislamu) wangeulizwa kwa nini makubaliano hayo yanaendelea na ni kitu gani kitatokea kama yakisitishwa. Hakuna sababu ya kuyaelekeza mashambulizi haya kwa Viongozi wa Wakristu ilhali serikali iliyoanzisha utaratibu huo ipo.
Ninashauri sisi wengine tujitahidi sana kuchimbua ukweli na tujiepusha kutoa maelezo ambayo hata sisi wenyewe tunajua kuwa si sahihi.
Hivi niulize kitu.. Kwa nini ndugu zangu wakristu mnapenda sana kutunga Uongo? Hivi kweli ndio mnaita ujanja wa waloelimika au mnataka tu kubishana..
Hivi kweli wewe uaamini shule zilijengwa wakati wa Muingereza tu ukasahau kwamba kulikuwa na Mjarumani kabla ya Muingereza? Sasa pengine pitia kipande hiki:-
In 1884 and 1885, Carl Peters and agents of the German East Africa Company made treaties with the Tanganyika main-land chiefs, and. in 1887 officials arrived to establish a colonial rule which lasted until 1914. The primary task of these administrators was to maintain law and order and develop communications which would open up the country to trade and commerce.
Missionaries proceeded the administrators and as education was an inevitable concomitant of evangelization, a system of rudimentary schools was quickly established. In 1900, there were 600 mission schools with 50,000 pupils accounting for 95% of the total school enrolment at the time, and by 1914 these figures had risen to 1000 schools with 150,000 pupils.
The Germans had no initial plans to establish an education system, but the need arose for them to train a junior and local civil service to staff their administrative machine. The purpose of their schools was thus defined in an official circular of 1903 as:
a. to enable the native to be used in government administration;
b. to inculcate a liking for order, cleanliness, diligence and dutifulness and a sound knowledge of German customs and patriotism
In single-minded fulfilment of these aims, they had established by 1914, 60 three-year village primary schools, 9 two-year central schools and one high school in Tanga providing clerical, industrial and teacher training for up to 500 pupils. The system was secular and strictly vocational but effective, and brought much favourable comment from British administrators who tried to rebuild the civil service in the 1920s.
Source
Mkuu wangu unakuwa kama hujui kiingereza. Hivi inaposemwa Administrator ina maana ndiye alojenga au ku administor? Je unataka kunambia pasipo Utawala wa Mjarumani bado hawa wachungaji wangeweza kufungua hizo shule na Hospital au umesahau Historia mkuu wangu. Halafu kama unakumbuka mwanzoni waloingia nchini sio serikali isipokuwa wafanya biashara kina Carl Peters wakijita explorer na kampuni yao waliyoiita Germany East Africa wakaja kabidhi nchi kwa serikali ya Ujarumani mwaka 1891..Mkandara,
Kazata hajasema uwongo. Hapo kwenye red unasoma mwenyewe kuwa missionaries proceeded the administrators lakini hii haina maana kwamba hela walizotumia administrators ndizo hizo hizo walizotumia wamishenari. Kumbuka nchi zote za Ulaya pamoja na Marekani zinafuata mfumo wa kutenganisha kanisa na serikali. Hizi misheni zilikuwa zinajitegemea. Uingereza na Marekani walikuwa na church mission societies ambazo zilichangisha hela zilizotumika kuanzisha makanisa, shule na hospitali katika makoloni walikokwenda. Hakuna hela ya serikali, ama ya mkoloni au ya koloni, kama anavyoamini Sadeeq, iliyotumika kuanzisha shule, makanisa na hospitali katika Tanzania. Hakuna. Kwa mfano kanisa letu pale Musoma, Mennonite, lilianzishwa na wamishenari kutoka Salunga, Pennsylvania, na mpaka leo wana kitengo cha Mennonite Church charities ambacho huchangisha hela zinazotumika popote pale duniani kunapokuwa na mahitaji ya kanisa lao. Sijui nimeeleweka?
Mkuu wangu unakuwa kama hujui kiingereza. Hivi inaposemwa Administrator ina maana ndiye alojenga au ku administrate? Je unataka kunambia pasipo Utawala wa Mjarumani bado hawa wachungaji wangeweza kufungua hizo shule na Hospital au umesahau Historia mkuu wangu. Halafu kama unakumbuka mwanzoni waloingia nchini sio serikali isipokuwa wafanya biashara kina Carl Peters wakijita explorer na kampuni yao waliyoiita Germany East Africa wakaja kabidhi nchi kwa serikali ya Ujarumani mwaka 1891..Mkandara,
Kazata hajasema uwongo. Hapo kwenye red unasoma mwenyewe kuwa missionaries proceeded the administrators lakini hii haina maana kwamba hela walizotumia administrators ndizo hizo hizo walizotumia wamishenari. Kumbuka nchi zote za Ulaya pamoja na Marekani zinafuata mfumo wa kutenganisha kanisa na serikali. Hizi misheni zilikuwa zinajitegemea. Uingereza na Marekani walikuwa na church mission societies ambazo zilichangisha hela zilizotumika kuanzisha makanisa, shule na hospitali katika makoloni walikokwenda. Hakuna hela ya serikali, ama ya mkoloni au ya koloni, kama anavyoamini Sadeeq, iliyotumika kuanzisha shule, makanisa na hospitali katika Tanzania. Hakuna. Kwa mfano kanisa letu pale Musoma, Mennonite, lilianzishwa na wamishenari kutoka Salunga, Pennsylvania, na mpaka leo wana kitengo cha Mennonite Church charities ambacho huchangisha hela zinazotumika popote pale duniani kunapokuwa na mahitaji ya kanisa lao. Sijui nimeeleweka?