Makanisa mpunguze michango jamani. Hasa RC, kuna nini siku hizi?

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
16,852
16,750
Hi, Salamu sana, 2018 is just few hours zimebakia..!!

Kama kuna kitu kimoja kimeniudhi mno mnooo 2017 ni michango ya kanisa.. Yaani imezidi sana sanaaa ni balaa, i feel bad, hasa RC yaani ni kerooo ( Sadaka za jpili hazina shida, this must be very clear, nasemea michango, tusichanganye hapa )

Michangooo michangoooo yaani huku unatoa sadaka ila bado unapewa mabahasha kama ya michango ya harusi.. Au SACCOS, inakera sana aiseee.. Tena sana

1: Kuna sadaka ( za kufuatwa majumbani)

2: Kuna michango lukuki ya Jumuia

3: Kuna michango ya Mtoto Yesu during Christmas

4: Kuna michango ya kila mwaka kwa kila mwanaume RC..

5: RC mfano Segerea, kila mwanaume atachangishwa ktk Jumuia 4,000 kila mwezi ya sadaka yaani kwa mwaka inatakiwa utoe 48,000

7: Ujenzi sijui Shule, Hospitali, Ukumbi, 2017 nimelipa 75,000 ya Ukumbi pekee..

8: Kila Jumapili kabla ya kumalizia misa kuna matangazo ya michango ni mingiii hadi keroooo yaani ni helaaa helaaaa helaaaaaaa helaaaaaa but wataita majina tofauti tofauti.. Na hapa nimetaja michango michache mno mnoo.. Najua wengi humu mnaenda kanisani mnalijua hili, tuwe huru tuseme sasa mmezidi, kama ni hela hata sisi tunazitaka pia, ila makanisa yamezidi mno michango.. Ni kero kabisa.. Let's speak it out!!

9: Hayo makanisa feki mengine ya mtu binafsi binafsi na familia yake eg Kakobe, Mwingira, Rwakatare, Mzee wa Upako, Gwajima, GeoDavi, TAG, sijui Mtume nani na nani, hao ndio haswa business as usual, matapeli wakubwa.. Yaani hawa siwasemi sbb wako wazi wao ni hela tu na kanisa ni mali yao private business.. Yaani ni enterprise yao, yaani iko wazi they do business, hata kuyaita KANISA haifai, ni ngumu au haikupaswa, sote tunajua kwa uwazi maisha ya kitajiri kupindukia wanayoishi hawa wamiliki binafsi wa haya makanisa feki, kuanzia magari ya kifahari, majumba ya kifahari, mabenki, ndege, maisha yao binafsi ni kufuru, ni ufahari kupindukia, wengine tabia zao social life mnazijua ni chafu sana, wengine wanaigiza ( Miracle Fiction ) kwa uwazi eti wanafufua watu, wengine wanawaambia ukitoa hela nyingi kwao ndio UTAPATA HELA NYINGI ZAIDI, wengine hata wanasema wana hela kuliko hata serikali, hii ni sababu wanalalia na kuamkia hela tu, kufuru imepitiliza!! Anyway hawa tuwaache we know kwa uwazi ni 100% business tu..!! Tuwaache sababu naamini Bwana wetu Yesu Kristo ata deal nao siku zao zikifika..!! Kuweni macho saa zote, acheni kulala, tumia ubongo wako vema.!!
These are what they do kwa hizo fake private churches ( Fiction, fiction tupu ).. tazama kwa umakini hii You Tube Watch..!!


Ila
RC au Anglican au KKKT au Moravian ni makanisa hayakuwa na mfumo huu wa kukusanya hela kwa kiwango hiki kupitia michango mingi mno ( hapa siongelei sadaka za jpili hizo hazina shida, naomba niweke wazi hili nasemea michango mingi isiyo na mwisho ), na haya ni public churches..

Kuna nini jamani makanisani? What is going around, where are we heading? Je tumepoteza msingi mkuu wa sala zetu na kuweka hela ( michango mingi ) mbele mno ndio imekuwa kama sala? Something is very very wrong..!! Je Bwana Wetu Yesu Kristo alitufunza hivyo? Miaka 10 nyuma 2007 hivi kurudi nyuma haikuwa hivi.. Sasa ni keroooo na usipochanga sahau kubatiziwa mtoto wako au kufungiwa ndoa au Kipaimara etc etc. Yaani ni kama vile kukomoana sasa.. RC & other churches maswala ya michangooo helaaa helaaa plseee plseee angalieni upyaaa.. Ni keroo sanaa

Kwani hizi hela siku hizi imekuaje? Jamani, najisikia vibaya sana.. Na wengi wanalalamika mno.. Aaaarrghh

2018 i hope mta change your trajectory kabisa kuhusu michangooo.. Aaaarghh

Bwana Yesu.. hakuchangisha watu hivi.. Si tunaishi kwa mfano wake sio.. Sasa michangooooo mahelaaa ya nn? Tuishi kama Bwana wetu Yesu Kristo.. Hii michango ndio watumishi wengine wanajengea private homes zao za kifahari ( mansions, villas ) na mabia & wines kila jioni kutumia michango yetu, hapana aiseee, only SADAKA tu nitatoa, full stop, michango sitoi kabisa tena nitasema kwa ukali wazi wazi.. byee byee michango yote..!! ( Sadaka ni sadaka na isije watu wakachanganya kusema ni michango, hapa naongelea michango mingi isiyoisha sio sadaka, hili liwe wazi kabisa, sadaka ya jpili haina tatizo ukitoa au usipotoa, tatizo narudia ni michango lukuki isiyo na mwisho )

2018 onwards sitaki utumwa tena sitakii.!!

Utumwa mwisho.. Sitakiii..!!
 
Kwani ni lazima kutoa? Kutoa ni moyo unaweza usitoe mchango wowote na ukaendelea kusali. Michango ya makanisani ni hiyari badala ya kuja kulialia hapa katafute pesa umtolee Mungu wako. Mungu anasema watu wangu wananiibia hawanitolei zaka. Kama mchango wa kawaida tu unalalamika je utaweza kutoa zaka(fungu la kumi)? Yaani ukipata milioni tano kwa mwezi umtolee Mungu laki tano utaweza?
Acha kumuibia Mungu
 
Si uache ukae bila dini kama unaona kero!Miaka ya nyuma makanisa yalitegemea wahisani ambao ni kutoka Ulaya na Asia sasa hivi hawatoi tena nao wamechoka,wahisani waliobakia ni waumini wenyewe sasa wewe unategemea kanisa linengwe na nani kama sio wewe muumini?kama unaona vipi achana na makanisa baki ulivo tuu bila kuwa na upande wowote wa kuabudu kisa michango faida yake utaiona tuu
 
Toa tu maana ndio namna ya kuitegemeza kazi ya Mungu na michango haitaisha mpk Yesu arudi

Cha msingi hiyo michango iwe kweli inatumika kwa kazi ya injili ila kama inaishia mifukoni mwa watu hiyo ni habari nyingine, inabidi muwaombe viongozi tu wawape taarifa ili kuweka uwazi wa mapato na matumizi
 
Si uache kwenda. Hizi tabia za kulalamika lalamika wabongo ni kama tumezaliwa nazo.

Mteja anakuja ananiambia "we jamaa siyo kabisa sasa ndiyo nini vitu kwenye flash havionekani, mbona hii hapa vinaonekana?" Badala aje tu aseme "Ebwana flash haionyeshi kitu, nichekie ishu ni nini"

Mwanao anakuja "Baba shule wamesema nikanyoe halafu mi njaa inauma naomba hela" tone nzima ni ya kulalama shenzi
 
Kwani ni lazima kutoa? Kutoa ni moyo unaweza usitoe mchango wowote na ukaendelea kusali. Michango ya makanisani ni hiyari badala ya kuja kulialia hapa katafute pesa umtolee Mungu wako. Mungu anasema watu wangu wananiibia hawanitolei zaka. Kama mchango wa kawaida tu unalalamika je utaweza kutoa zaka(fungu la kumi)? Yaani ukipata milioni tano kwa mwezi umtolee Mungu laki tano utaweza?
Acha kumuibia Mungu

Acha mental slavery..!!
Nani kakwambia ni hiari siku hizi michango usipotoa sahau huduma za kanisa.. Siongelei sadaka, nasema michango..
Unajua zaka tunatoa za kila jpili and jumuia tunatoa sana hadi unga, mchele tunachanga.. But inakuwa kerooo kerooo sanaaa sbb wanazidisha michango kuliko kawaida.. Ni mingi mnoo.

Kanisa lina vitega uchumi vingi tu sana, sadaka za jpili zingewatosha sana sana.. Ila wanamichango mingiii mnoo
 
Kwani ni lazima kutoa? Kutoa ni moyo unaweza usitoe mchango wowote na ukaendelea kusali. Michango ya makanisani ni hiyari badala ya kuja kulialia hapa katafute pesa umtolee Mungu wako. Mungu anasema watu wangu wananiibia hawanitolei zaka. Kama mchango wa kawaida tu unalalamika je utaweza kutoa zaka(fungu la kumi)? Yaani ukipata milioni tano kwa mwezi umtolee Mungu laki tano utaweza?
Acha kumuibia Mungu
Ndugu siku hizi siyo hiari usipo toa hupati huduma zozite za kiroo kanisani anachokisema ndugu yetu ni ukweli mtupu
 
Unasema makanisa kama ya kina Kakobe ni biashara halafu unasema RC kama hujato michango sahau kubatiziwa mtoto, tofauti ni nini kati ya Kakobe na RC kama hata kubatiza mtoto lazima ulipe hela?

Kubatiza ulipe hela, kubariki mtoto ulipe hela, kubariki ndoa ulipe hela, michango ya ujenzi wa shule(ingawa mwanao hawezi kupewa discount ukimpeleka hapo pamoja na kwamba ulichangia ujenzi),hospitali, ukumbi, kumbariki padri na mamichango kibao alafu unasema sio kama kina Kakobe?

Sisi wengine tulishashtukia huu mchezo wa dini miaka mingi sana kua ni ulaji wa viongozi na wala hakuna kitu kinaitwa Mungu wala shetani ni uhuni tu.

Cha ajabu unakuta mtu anawacheka waumini wa Kakobe kua wanaibiwa, yeye hajioni kama anaibiwa na labda anaibiwa zaidi. Hivi siku hizi ile hela ya kutoa usamehewe dhambi na padri imeondolewa? Eti padri au askofu anasamehe dhambi!!!
 
Back
Top Bottom