Kwanini kwenye makanisa ya kilokole, kisabato hakuna ombaomba nje kama Misikitini?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,370
Wasalaam,

Nimechagua hawa maana ndio wanavuguvugu kubwa la kuliishi neno. Sina uzoefu na RC au KKKT lakini makanisa ya kisabato na kilokole mengi nimeingia.

Tofauti na wale wakristo wa awali, Njia ya kuelekea hekaluni ilikuwa imejaa ombaomba. Hawa jamaa walikuwa wanamvizaga Yesu, mitume wanapoingia kuabudu angalau wapate chochote.

Siku hizi hii kitu haipo, tatizo ni nini

Uchoyo umezidi?

Wananjia kificho ya kusaidia masikini?

Wachungaji wanahofu mizigo isijeishia njiani hivyo hufukuzwa kwenye mzingo wa kanisa.

Tofauti na Waislam kuna siku maalum unaona watu wanakuja kugawiwa misosi, pesa, na sadaka mbalimbali

Tatizo ni nini?

No hayo tu.
 
Siyo vizur kupokeapokea ovyo,watu wanagawa misaada kwa maagano Yao,ni heri kutoa kuliko kupokea ina maana kubwa sana
 
Kuna msikiti nimeona Tabora kila ijumaa kila mtu haijalishi dini anatoka na kilo mbili unusu ya nyama
 
Hamuoni Yanga walikua wanatoa msaada,,huku Mayele analia kutupiwa vitu,,,,,,,misaada mingine watu wanapunguza tu karma za mabaya yao
 
Makanisa ya kilokole wachungaji ndio omba omba , waumini wanajimaliza huko , omba omba wengine wameona kwenda humo ni kuleta mgongano wa kimaslai tu.
 
Ukiingia kanisani unapata msaada zaidi hutokua ombaomba tena.
Utaishi kwa raha mustarehe maana kuna muumini atajtolea kukuhudumia.
 
Sasa kanisa limezunguukwa na geti kubwa kuna mlinzi, wanaoingia na kutoka wako kwenye magari,

Wakati msikiti uko kwenye kona fulani hivi af wanatoka wanapiga one two one two hadi home.

Accessibility brother
 
Wasalaam,

Nimechagua hawa maana ndio wanavuguvugu kubwa la kuliishi neno. Sina uzoefu na RC au KKKT lakini makanisa ya kisabato na kilokole mengi nimeingia.

Tofauti na wale wakristo wa awali, Njia ya kuelekea hekaluni ilikuwa imejaa ombaomba. Hawa jamaa walikuwa wanamvizaga Yesu, mitume wanapoingia kuabudu angalau wapate chochote.

Siku hizi hii kitu haipo, tatizo ni nini

Uchoyo umezidi?

Wananjia kificho ya kusaidia masikini?

Wachungaji wanahofu mizigo isijeishia njiani hivyo hufukuzwa kwenye mzingo wa kanisa.

Tofauti na Waislam kuna siku maalum unaona watu wanakuja kugawiwa misosi, pesa, na sadaka mbalimbali

Tatizo ni nini?

No hayo tu.
Sasa kama mchungaji mwenyewe omba omba unategemea kuwe na omba omba wengine nje?
 
haya ilipofika saa,petro na yohana walikwea hekaluni,nje ya vizimba wakakutana na mhitaji asiyejiweza kwa maradhi akiomba,alipowaona aliimba msaada maana zoezi la kutiwa birikani lilikuwa gumu sana kwake na amekuwa akijaribu kipindi kirefu sasa bila mafanikio.
mabwana wale kwa kujua nao pia ni apeche alolo wakamwambia"hatuna pesa za kukupa,lakini pokea hiki tulicho nacho,kwa jina la Yesu simama uondoke umetakasika"jama akapona kabisa kuanzia pale.

kimsingi omba omba anatakiwa asaidiwe aache kuomba omba,kwa kupewa matibabu kama anaumwa ama apewe mtaji kama uchumi ni mbovu.
 
Wasalaam,

Nimechagua hawa maana ndio wanavuguvugu kubwa la kuliishi neno. Sina uzoefu na RC au KKKT lakini makanisa ya kisabato na kilokole mengi nimeingia.

Tofauti na wale wakristo wa awali, Njia ya kuelekea hekaluni ilikuwa imejaa ombaomba. Hawa jamaa walikuwa wanamvizaga Yesu, mitume wanapoingia kuabudu angalau wapate chochote.

Siku hizi hii kitu haipo, tatizo ni nini

Uchoyo umezidi?

Wananjia kificho ya kusaidia masikini?

Wachungaji wanahofu mizigo isijeishia njiani hivyo hufukuzwa kwenye mzingo wa kanisa.

Tofauti na Waislam kuna siku maalum unaona watu wanakuja kugawiwa misosi, pesa, na sadaka mbalimbali

Tatizo ni nini?

No hayo tu.
Kuwepo kwao humo,walishakaushwa damu,na kausha damu wa humo,hivyo hawana hata ya kuwasaidia ombaomba 😅
 
Back
Top Bottom