February 17, 2020
FULL HISTORIA YA MAMA SAMIA
Mama Samia anakubali hoja nzito za wapinzani, nilikataa pendekezo la kuwa Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu asema kilichomsukuma kuingia katika siasa ni maoni na hoja za mashiko za wapinzani Bungeni / Baraza la Wawakilishi ambazo hazijibiwi vyema kwa hoja na mawaziri wa serikali.
Hilo la kukerwa na majibu ya serikali yasiyokidhi hoja za wapinzani, Mama Samia akajiona ni kama Activist / Mwanaharakati ingawa ni CCM anayehusudu maswali magumu yajibiwe kwa hoja thabiti.
Mama Samia anaongeza kabla ya kuingia siasa alikuwa anaona nondo za wapinzani huku upande wa serikali ambayo ni ya CCM bara na Visiwani pia, mawaziri huja na majibu hafifu yasiyo ridhisha kwake na wanaofuatilia shughuli za Bunge.
Pamoja na kukunwa na hoja zilizoenda shule za wapinzani, Mama Samia aliwaeleza wasikilizaji ametokea ktk familia ya kawaida ambapo baba yake alikuwa mwalimu wa shule na mama yake mama wa nyumbani aliyetumia nafasi kuwafundisha na kuwasaidia kazi za masomo wakitoka shule.
Hiyo ilimsukuma kujiendeleza kimasomo kila wakati na kufanya kazi katika serikali ya SMZ na muda mrefu katika NGO's mbalimbali za kimataifa kabla ya kujiunga na siasa kupitia viti maalum CCM.
Mama Samia alipofanikiwa kuteuliwa Mwakilishi wa Viti Maalum alipata faraja kubwa akitegemea kutasaidia kukijenga chama cha CCM kuwa na watendaji wajibu-hoja-wazuri, kutokana na kuona mawaziri wa serikali na wabunge wa CCM kukosa hoja motomoto au majibu yakuridhisha kwa maswali na hoja nzuri za wapinzani na kuzidiwa wakiwa bungeni au baraza la wakilishi wakionekana / kusikika 'live' .
Ghafla bin vu, Mama Samia alipoingia Baraza la Wakilishi akateuliwa kuwa Waziri wa Sera Ajira Maendeleo ya akina Mama na Vijana ktk Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Na miaka 5 baadaye akawa waziri wa Biashara na Utalii katika SMZ. Baadaye akagombea kiti Makunduchi Zanzibar na kufanikiwa kuwa mbunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuteuliwa kuwa Waziri wa Mazingira na hatimaye mgombea Mwenza wa Urais na kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Hakutegemea kupewa nafasi hizo ghafla hivyo na pia akikumbuka nondo za wapinzani bungeni kupitia maswali, akaona amewekwa mstari wa mbele kukabiliana na hoja zinazowagusa wananchi ambazo hazipatiwi majibu ya kuwaridhisha wananchi.
Source: Millard Ayo