Makamu wa rais, Mama Samia Suluhu kuwa ngangari kidogo katika kauli zako

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,732
Habari zenu!
Makamu wa rais sijui ni ukarimu wa kupitiliza ule wa wazanzibari, leo wakati akitoa amri kwa mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya kuwa anapiga marufuku shughuli za kibinadamu kufanyika ktk bonde la mto Ruaha, anatoa amri kwa upoooooooooole, yaani hata hao anaowaamrisha watakuwa wanadharau, ongea kwa mamlaka madam watu wakuelewe!
Acha kutoa amri za kubembeleza!
 
amri za ukali kutoka na raia namba moja zinatosha, mama endelea kutubembeleza wanao tunapokuwa tumekata tamaa na kauli za baba mwenye nyumba na wapendwa wake DAB na Gamboshi
Amri inatekelezwa vizuri kama kauli yako ya amri inakuwa sambamba na amri, onyesha kweli kuwa unatoa amri, simaanishi afoke!
 
Dah! Kiukweli mimi huwa nasikia raha kweli namna anavyoongea kwa kubebembeleza wallah huyu makamu namuelewa sana.
 
Aseeeh hatari sana..watendaji husika watatilia maanani agizo lake usijali mkuu
 
Kuwa na moyo wa kiasi ni busara.
Mh.Makamu wa Rais Samia Suluhu endelea hivyo hivyo na utendaji usio na misimamo mikali.
Kwa mfano wale waliovamia vyanzo vya Maji MTO Ruhaa Mkuu,maamuzi uliyafanya yako very balance.
 
Dah! Kiukweli mimi huwa nasikia raha kweli namna anavyoongea kwa kubebembeleza wallah huyu makamu namuelewa sana.


Mkuu hata mimi napenda sana kumsikia akiongea. Anatumia lugha fasaha na nyepesi kabisa. Hadi raha kumsikiliza.
 
Back
Top Bottom