Makamu Wa Rais Kuongoza Ujumbe Wa Tanzania Katika Sherehe Za Kuapishwa Kwa Rais Mteule Wa Burundi June 18,2020

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1592403689648.png


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Nchini Burundi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Burundi Mhe Evariste Ndayishimiye hapo kesho June 18,2020.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo Jijini dar es Salaam katika Ubalozi wa Burundi Nchini Tanzania alipokwenda Ubalozini hapo kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza aliyefariki June 09,2020 kwa maradhi ya Moyo.

Ameongeza kuwa kutokana na mahusiano ya karibu yaliyopo baina ya Burundi na Tanzania Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamua kuongeza ujumbe wa Tanzania kwenda Burundi ambapo mbali na kuongozwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pia ataambatana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Prof. Kabudi amesema kuwa Hayati Pierre Nkurunziza amefanya kazi kubwa sana ya kuiunganisha Burundi na kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi zenye umoja na amani katika bara la Afrika lakini pia kuirejeshea Burundi matumaini na amani ya demokrasia na kudhihirika katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka huu na kumalizika kwa amani.

Kwa upande wake Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Balozi Gervais Abayeho amesema Ubalozi huo na Warundi kwa ujumla wamepokea kwa mshtuko na majozi taarifa za kifo cha Rais Pierre Nkurunziza hasa ukichukulia kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi Rais huyo alikuwa akiendelea na shughuli zake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi.
 
6e1d9b01b7d808b81507dd00a293e2d4

Evariste Ndayishimiye, Rais mpya wa Burundi
EVARISTE Ndayishimiye, rais mteule wa Burundi anatarajiwa kuapishwa kesho tarehe 18 Juni 2020, badala ya Agosti kama ilivyopangwa.

Tume ya Uchaguzi ya Burundi wakati wa mchakato wa uchaguzi, ilileleza kwamba rais atakayechaguliwa na wananchi, ataabishwa Agosti, ratiba hiyo imebadilishwa baada ya kicho cha ghafla cha rais wa taifa hilo, Pierre Nkurunziza.
Imeelezwa, Ndayishimiye angeweza kuapishwa iwapo Nkurunziza angekuwa hai, lakini sasa nchi haina rais na si busara kusubiri wakati huo wakati hakuna kikwazo chochote kwa sasa.
Ndayishimiye anayetokana na chama tawala wa CNDD-FDD, ataapishwa katika Mji wa Gitega ikiwa ni wiki moja baada ya mtangulizi wake kufariki dunia kwa mshtuko wa moyo.

Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 Juni 2020. Baada ya kuapishwa, Ndayishimiye atahudumia taifa hilo kwa kipindi cha miaka saba.
 
Kila laheri kwake, wamefanya vyema maana si afya kwa nchi kukosa kiongozi Mkuu.
 
Back
Top Bottom