Makamu wa Rais Dkt. Mpango akutana na Dkt. Nchimbi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, amekutana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, mapema leo Jumatatu, tarehe 28 Aprili 2025.

Dkt. Mpango amewasili nchini akitokea Vatican, ambako alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Hayati Baba Mtakatifu Papa Francis.

publer-1745857013164.jpg
publer-1745857007963.jpg
 
Attachments

  • publer-1745857011507.jpg
    publer-1745857011507.jpg
    57.3 KB · Views: 36
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, amekutana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, mapema leo Jumatatu, tarehe 28 Aprili 2025.

Dkt. Mpango amewasili nchini akitokea Vatican, ambako alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Hayati Baba Mtakatifu Papa Francis.

Siku zote hizo alikuwa Vatican anafanya nini na papa alishazikwa au anaosha vyombo?
 
Katika hali ya kawaida, hawa ndio wangekuwa wameshikilia maslai ya nchi hii mikononi mwao wakati huu; lakini inasikitisha kwamba wanatumika tu kama vikaratasi vya chooni vya kusafishia uchafu.
Inaudhi sana.
 
Mbona nasikia afya yake siyo nzuri sana na alikuwa ameomba kujiuzu wakamwomba amalizie ungwe?
Ni wazi afya yake siyo nzuri, tokea wakati ule wa COVID- alipoponea chupu chupu. Ni muujiza tu kwamba huyu ali-survive; lakini 'damage' ilikuwa kubwa.

Hata hivyo, ni wazi kwamba Philipo ni "technician' zaidi kuliko mwanasiasa.
Haiba yake haiendani kabisa na siasa.
 
Sio kweli inasemwa hawapikiki chungu kimoja na malikia sheba 😁
Kama huyu hapikiki naye huyo anayekuja atawezana naye? Si anaonekana kama mjanja mjanja kisiasa kuliko huyu? Kuna uwezekano dirisha lile lile lililotumiwa na malkia kuingia ndani na yeye akalitumia.
 
Katika hali ya kawaida, hawa ndio wangekuwa wameshikilia maslai ya nchi hii mikononi mwao wakati huu; lakini inasikitisha kwamba wanatumika tu kama vikaratasi vya chooni vya kusafishia uchafu.
Inaudhi sana.
Hili jambo la makamu kuwa president in waiting ni hatari sana. Wasipofanya marekebisho haraka naona makamu mwingine akiwa rais katikati ya kipindi.
 
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, amekutana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, mapema leo Jumatatu, tarehe 28 Aprili 2025.

Dkt. Mpango amewasili nchini akitokea Vatican, ambako alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Hayati Baba Mtakatifu Papa Francis.

Hii sawa na Heche kukutana Lema kwa sababu wote ni chama kimoja
 
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, amekutana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, mapema leo Jumatatu, tarehe 28 Aprili 2025.

Dkt. Mpango amewasili nchini akitokea Vatican, ambako alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Hayati Baba Mtakatifu Papa Francis.

Vatican City
 
Back
Top Bottom